“Shindano hili limetungwa ili kuboresha ufundi wa kutengeneza filamu fupi zinazobuniwa na vijana wa Kiafrika”,
alisema Fabrizio Colombo, Mkurugenzi Msaidiziwa ZIFF. “Filamu 16
zimo katika kinyang’anyiro hicho, na washindi watatu watapewa $2000
kila mmoja ili kuwasaidia kutengeneza filamu nyingine tayari kwa tamasha la ZIFF mwaka ujao”
aliongezea.
Bernd
Multhaup washirika la GIZ, wadhaminiwatuzohii, alinakiliwa akisema,
“Tuliamuwa kutoa zawadi tatu ili kuwapa motisha watengeneza filamu wengi zaidi kwa kupitia tuzo ya Sembene.
Tunatambua kuwa filamu fupi zinauwezo mkubwa wa kuboresha ubunifu bila ya kupunguza ubora wa filamu”.
Hao washindi watatu watatakiwa kutuma hadithi zao pamoja na mpango-kazi
wautengenezaji wa hizo filamu kabla hawajapewa fedha walizoshinda ilikuhakikisha filamu zitatengenezwa kuwahi tamasha lijalo mwakani.
Kwa njia hiyo ZIFF itahakikisha kupata filamu nyingine na kuboresha
ufundi wa kutengeneza filamu fupi na
bora.
Filamu
16 zilizochaguliwani:
Lesley: Victor
Okoye Frank, USA / 15 min
O Canto da
Iona: Thiago B. Mendonca, Brazil / 25 min
Maruna: Molly
Kane, Senegal / 15 min
Aisaa’s Story:
Iquo B Essien, USA / 15 min
Madama Esther:
Luck Razanajaona, Madagascar / 15 min
The Traveller:
Victoria Dogbe, Ghana / 9 min
Damaru:
AgborObed, Cameroon / 24 min
Houkak:
YounesYoufsi, Morocco / 17 min
Kwaku: Anthony
Nti, Ghana / 16 min
SamakiMchangani:
AmilShivji, Tanzania, 30min
Kilimo 2:
Neema& Warren Reed, Tanzania / 6 min
LiberteEmprisonnee:
Sara Mikayel, Senegal /16min
SokoSonko:
EkwaMsangi, Kenya / 22 min
Uthando:
TulananaBohela, South Africa, 20min
Grandma Knows
Best: Tamara Dawit, Ethiopia, 16min
Vitrin, Regis Talia, Cameroon, 15min
JuuYaMradi:Mradi huu unadhaminiwa na
GIZ,shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani ambalo linasaidia Tanzania
na Jumuiaya Afrika Mashariki. ZIFF
ni tamasha kubwa kuliko yote Afrika mashariki na ambalo linatambuliwa kimataifa.
Tamasha linadhaminiwa na ZUKU kupitia mkataba waudhamini wa miaka 10 utaoisha 2021.
No comments:
Post a Comment