4
Che Mundugwao enzi za uhai wake.

Katika masikitiko makubwa na majonzi, Tanzania imeweza kumpoteza msanii mahiri  wa muziki wa asili nchini, Chigwele Che Mundugwao  alifariki jana.

Matukio ya nyuma kupotea kwenye muziki kwa Che Mundugwao!

chemundu
Awali Che Mundugwao ambaye  mwaka 2013, alikuwa akikabiliwa na kesi Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, wakikabiliwa na jumla ya mashitaka manne likiwemo kosa la wizi wa jumla ya Pasipoti 26.
Ilielezwa kuwa, Che Mundugwao, wakili Komanya alidai kuwa mshitakiwa huyo kuwa Aprili 22, mwaka 2013,  alikamatwa akimiliki  paspoti 12  za watu wengine bila ya kuwa na sababu yoyote ya msingi .
Ilieleza kuwa, Mei 2013,  Che Mundugwao pia alikamatwa na maofisa wanausalama akimiliki pasipoti nyingine mbili  zenye majina ya watu wengine sababu yoyote ya msingi.
Aidha, Che Mundugwao wakati wa uzima wake, aliwahi kuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Muziki na Mwenyekiti wa Chama cha muziki wa asili nchini.
Ambapo katika kuakikisha muziki wa Tanzania, mara  kwa mara alikuwa akiwataka wadau wa muziki kuwa na alama ya pamoja ambayo itatambulisha Taifa kufahamika, tofauti na sasa mtu anaimba rege lakini baadae utakuta huyo huyo anaimba zuku ama mchiriku.
Pia aliwahi kutwaa tuzo za msanii bora wa nyimbo za Asili za Kilimanjaro Kill Award, miaka ya nyuma.
Tunaungana na watanzania wote pamoja ndugu jamaa na marafiki wakiwemo wa tasnia ya muziki hapa Nchini katika kipindi hiki kigumu cha majonzi, Mungu amlaze mahala pema pa milele, Amen.