Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars) ijumaa ya tarehe 10, Aprili mwaka huu, itashuka dimbani Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuwakarisbisha timu ya Taifa ya Wanawake ya Zambia (The She-Polopolo).
Twiga Stars inayonolewa na kocha mkuu Rogasian Kaijage iliingia kambini mwishoni mwa wiki na kikosi cha wachezaji 25 katika hostel za TFF zilizopo Karume, kujiandaa na mchezo huo ambao ni muhimu wa kuwania kufuzu kwa fainali za michezo ya Afrika mwaka huu.
Katika mchezo wa awali uliofanyika wiki mbili zilizopita jijini Lusaka Zambia, Twiga Stars iliibuka na ushindi wa mabao 4-2, mabao yaliyofungwa na Asha Rashid (2), Shelder Boniface (1) na Sophia Mwasikili (1).
Mshindi wa jumla katika mchezo huo atafuzu moja kwa moja kwa fainali za Michezo ya Afrika zitakazofanya nc
No comments:
Post a Comment