Katika kuunga mkono kauli hiyo,
Malinzi amemwandikia barua Rais wa COSAFA Seketu Patel na nakala yake kwenda
kwa Dr. Danny Jordan Rais wa Chama cha Mpira nchini Afrika Kusini (SAFA)
akielekeze masikitiko yake juu ya mauaji na vurugu yanatokoea nchini humo.
Aidha Malinzi ameeleze imani yake
kuwa, kwa kushirkiana kwa pamoja nchi za Kusini mwa Afrika zitaweza kuutumia
mchezo wa mpira wa miguu kama kiunganishi cha vijana, na kipaza sauti cha
kuhamasisha utokomezaji wa ubaguzi wa uraia wa mtu.
Mapema jana Rais wa COSAFA, Seketu
Patel alisema nchini Afrika Kusini baadhi ya miji kumekua na taarifa ubaguzi, vurugu
na kutokea mashambulio zinazofanywa ili kuwataka wageni waondoke nchini humo,
ila wao kama COSAFA wamepanga kuitumia michuano hiyo kama sehemu ya kurejesha
amani na utulivu kwa wakazi huko.
COSAFA ni michuano inayojumuisha watu
kutoka katika mataifa mbalimbali, kuelekea kwenye michuano hiyo sie tupo nyuma
ya SAFA kuhakikisha michuano hiyo inafanyika na kurejesha amani na utulivu,
kuwafanya watu wote kuungana na kuwa kitu kimoja "alisema Patel"
Michuano ya COSAFA inatarajiwa
kufanyika mwezi Mei mwaka huu katika jimbo la Kaskazini-Magharibi (North-West
Province) ambapo hakujaathirika na mashambulio hayo, na serikali ya Afrika
Kusini imesema itahakikisha ulinzi na usalama unaendelea kuwepo na kuimarika
kwa hali ya juu.
Chama cha Soka nchini Afrika Kusini
(SAFA) kimelaani vurugu hizo zinazoendelea nchini humo na kusema wao kama
wenyeji wamejiandaa kuhakikisha michuano hiyo inafanyika kwa amani na usalama,
hata wakati wa Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini (2010), palikua na tishio la
hali ya usalama lakini michuano iliweza
kufanyika na kumalizika kwa usalama.
Aliyekua Rais wa Chama cha Soka cha
Nambia (NFA) John Muinjo, ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa kamati ya waamuzi wa
COSAFA na mjumbe wa muda mrefu amesema anaamini michuano hiyo itarudisha umoja
kwa watu wanaoishi nchini Afrika Kusini.
Michuano ya COSAFA inatarajiwa kuanza
kutimua vumbi Mei 17, 2015 katika jiji la Rusternburg (North-West
Province) nchini Afrika Kusini katika
viwanja vya Olympia Park na Moruleng ikishirikia nchi za Botswana, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius,
Mozambique, Namibia, Seychelles, South
Africa, Swaziland, Zambia and Zimbabwe.
No comments:
Post a Comment