Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, April 17, 2015

STAND UNITED KIBARUANI NA JKT RUVU LEO

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania inaendelea leo kwa mchezo mmoja, wenyeji timu ya Stand United kuwakaribisha maafande wa JKT Ruvu katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Ligi hiyo ya Vodacom itaendelea kutimua vumbi siku ya jumamosi  kwa michezo mitatu, mjini Morogoro wenyeji Polisi Morogoro watawakaribisha Ndanda FC kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Jijini Mbeya wenyeji timu ya Mbeya City watawakaribisha timu ya Simba SC kwenye uwanja wa Sokoine , huku Azam FC wakiwakaribisha wakata miwa wa Kagera Sugar kwenye uwanja wa Chamanzi Complex.

Jumapili Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania itaendelea  kwa maafande wa timu ya Ruvu Shooting  kuwakaribisha maafande wenzao wa Mgambo Shooting katika uwanja wa Mabatini - Mlandizi, huku jijini Mbeya wenyeji timu ya Prisons FC wakiwakaribisha wakata miwa wa Mtibwa Sugar.

No comments:

Post a Comment