Katika
salamu zake kwa klabu ya Young Africans, Rais Malinzi amewaambia wanapaswa
kupambana na kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo wa jumamosi, ili
kujiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele katika mchezo wa marudiano
kwani ndio pekee kwa sasa wanaoipeperusha bendera ya Tanzania katika michuano
ya kimataifa.
Young
Africans imeingia katika hatua ya 16 bora Kombe l Shirikisho barani
Afrika,baada ya kuzitoa BDF XI ya Botswana katika hatua ya awali kwa jumla ya
mabao (3-2), kisha kuwaondoa FC Platinum ya Zimbabwe katika hatua ya kwanza kwa
jumla ya mabao (5-2).
Endapo
timu
ya Young Africans itafanikiwa kuwaondoa Etoile du Sahel itasuburia
kucheza mechi ya mtoano (Play-off) dhidi ya timu mojawapo
zitakaotolewa katika 16 bora ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika (CL).
Wakati
huo huo wapinzani wa Young Africans timu ya Etoile du Sahel wanatarajiwa
kuwasili saa 9 usiku kuamkia ijumaa kwa
usafiri wa Ndege ya kukodi ya kampuni ya Nouvelair bj 4870 wakiwa na msafara wa watu 56.
Makamu
wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tunisia (FTF), Bw. Krifa Jalel ndiye mkuu wa msafara
huo akiwa na Rais wa klabu ya Etoile du Sahel (ESS) Bw.Charefeddine Ridha,
wachezaji 19, benchi la ufundi lenye watu 13, waandishi wa habari 12 na
wanachama 10
Timu ya
Etoile du Sahel itafikia katika hoteli ya Ledger Plaza zamani Bahari Beach eneo
la Kunduchi, na kesho jioni ijumaa wanatarajiwa kufanya mazoezi katika uwanja
wa Taifa jijini Dar es salaam.
Waamuzi
wa mchezo huo ni Samwel Chirindiza, Arsenio Marenguka, Celio de Jesus Musabe,
Jose Maria Bachide wote kutoka nchini Msumbuji na wanatarajiwa kuwasili leo mchana,
huku kamisaa wa mchezo huo Salah Ahmed Mohamed kutokea nchini Sudan akitarajiwa
kuwasili leo jioni na wote watafikia katika hoteli ya Protea iliyopo Oysterbay.
No comments:
Post a Comment