Michuano ya soka kwa ligi ya wanawake mkoa wa Dar es salaam
inaanza kutimua vumbi jumapili hii ya April 19/2015,kwa vilabu mbalimbali
kuchuana vikali kuuwania ubingwa huo.
Kwa mujibu wa kamati ya mashindano ya chama cha soka mkoa wa
Dar es salaam DRFA,maandalizi kuelekea michuano hiyo yamekamilika ikiwa ni
pamoja na viongozi wa vilabu husika kupewa kanuni na taratibu zitakazotumika
katika mashindano.
Jumla ya vilabu vinane (8) vitashiriki katika ligi hiyo ya
wanawake,ambavyo ni SIMBA QUEENS, REAL TANZANITE, TEMEKE SQUAD, EVER-GREEN
QUEENS, JKT QUEENS,LULU QUEENS, MBURAHATI QUEENS na UZURI QUEENS.
Mechi ya ufunguzi itazikutanisha timu za Temeke Squad dhidi
ya Ever-Green Queens,itakayopigwa katika uwanja wa Mwalimu Nyerere Kinondoni
jijini Dar es salaam Jumapili ya April 19.
No comments:
Post a Comment