Kikosi cha Simba |
Mashabiki Simba |
Mshambuliaji wa Simba, Elias Maguri akijaribu kuwahi mpira huku beki wa Yanga akiwa chini |
Kikosi cha Yanga |
Benchi la Yanga baada ya mchezo kumalizika |
Makocha wakipongezana baada ya mchezo kumalizika |
Add captioMashabiki wa Yanga |
Kampeni ya Imetosha nayo ilihamia Taifa kwa ajili ya kuwahamasisha mashabiki kuhusiana na kuacha vitendo vya unyanyapaa na vifo vya watu wenye ulemavu wa ngozi |
BAO la dakika ya 51 lililofungwa na mshambuliaji Emmanuel
Okwi, lilitosha kuipa pointi tatu timu ya
Simba iliyokuwa ikipambana na Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya
Tanzania bara uliochezwa uwanja wa taifa Dar es Salaam.
Ushindi huo unakuwa wa pili mfululizo kwa Simba ambayo wiki
iliyopita iliweza kuifunga Tanzania Prisons mabao 5-0 na sasa imefufua
matumaini ya kuwania ubingwa baada ya kufikisha pointi 26 katika nafasi ya tatu
huku Yanga wakiendelea kubaki kileleni na pointi zao 31.
Katika mchezo huo Simba ilionyesha daliliza ushindi tangu
mwanzoni baada ya kutawala mchezo huo hasa eneo la kiungo kwa dakika 20 huku
Yanga wakionekana kucheza kwa kujihami na kutumia mashambulizi ya kustukiza
ambayo hata hivyo hayakuwa na madhara kwa wapinzani wao.
Mshambuliaji anayechipukia kwa kasi wa Simba alikuwa wa
kwanza kulifikia lango la Yanga katika dakika ya pili na kuachia shuti kali
ambalo halikuweza kulenga lango na kutoka nje.
Simon Msuva angeweza kuifungia timu yake ya Yanga bao la
kuongoza dakika ya saba baada ya kupata nafasi nzuri akiwa ndani ya 18 lakini
chakushangazabaada ya kumtengenezea Amissi Tambwe afunge alipiga shuti dhaifu
lililodakwa na kipa wa Simba Ivo Mapunda.
Kadri muda ulivyokuwa ikienda Yanga ilionekana kuimarika na
kurudi mchezoni na kuanza kuutawala mchezo na kutengeneza nafasi nyingi ikiwemo
ile ya dakika 25 aliyoipata Danny Mrwanda lakini alipatwa na kigugumizi cha
muguu na kushindwa kufunga.
Dakika tano baadaye kocha wa Yanga Hans van der Pluijm
aliamua kumtoa nje Mrwanda na nafasi yake kuchukuliwa na Hussein Javu , hiyo
ilitokana na mchezaji huyo kuonyeshwa kadi ya njano baada ya kumuonyesha ubabe
beki wa Simba Kessy Ramadhani ambaye awali alimchezea rafu.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu hizo zilikuwa bado
hazija fungana na Yanga ndiyo waliopata nafasi tano za kufunga mabao kupitia
kwa washambuliaji wake Mrisho Ngassa, Simon Msuva, Tambwe na Mrwanda.
Kipindi cha pili kilianza kwa Simba kuanza kuliandama lango
la Yanga ambapo Ibrahim Ajibu, alipata
nafasi nzuri dakika ya 47 akiwa nje ya
eneo la hatari na kupiga shuti kali lilitoka nje na kuwa goli kiki.
Yanga ilijibu shambulizi hilo katika dakika ya 49 Javu aliyewapangua mabeki wa Simba na
kupiga shuti kali lililopanguliwa na kipa Mapunda na kuwa kona ambayo iliokolewa
vyema na mabeki wa Simba .
Mchezo huo uliendelea kuwa wa ushindani zaidi kwa timu zote
mbili kutafuta nafasi ya mabao lakini makosa yaliyofanywa na mabeki wa Yanga
kwa kushindwa kujipanga vyema yaliinufaisha Simba katika dakika ya 51 baada ya
Okwi kufunga bao hilo pekee akipokea pasi ya Ibrahim Ajibu na kumtungua kipa wa
Yanga Ally Mustapha ‘Bartherz’ aliyekuwa ametoka langoni mwake.
Baada ya kuingia kwa bao hilo Yanga walionekana kubadilika
na kucheza kwa kasi wakitafuta bao la kusawazisha lakini katika dakika ya 74
walijikuta wakicheza pungufu baada ya kiungo Mnyarwanda Haruna Niyonzima
kuonyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi Martin Saanya kwa kosa la kupiga mpira
wakati filimbi imeshapigwa.
Hiyo ilikuwa ni kadi ya pili ya njano awali Niyonzima alionyeshwa
kadi ya njano dakika ya 42 kipindi cha
kwanza kwa kumchezea rafu Ramadhani Singano.
Simba nayo baada ya kupata bao hilo ilionekana kucheza kwa
kupoteza muda huku ikifanya mashambulizi ya kustukiza na dakika ya 80 Okwi tena
alipiga shuti kali lilitoka pembeni kidogo ya lango la Yanga.
Kutokana na presha ya mchezo huo kwa nyakati tofauti
wachezaji wa timu zote mbili walionekana kuchezeana kibabe ambapo dakika ya 78
beki wa Simba Juuko Murshid na Amissi Tambwe walionyeshwa kadi za njano
kwa kuonyeshana undava.
Baada ya kuona mambo magumu kocha wa Yanga aliamua kumtoa
Ngassa na kumuingiza Kpah Sherman hwakati kwa uande wa Simba kocha Goran
Kopunovic aliwatoa Ibrahim Ajibu ambaye nafasi yake ilichukuliwa na Elias
Maguli na dakika ya 87 ilimtua Abdi Banda ambaye nafasi yake ilichukuliwa na
Simon Sserunkuma.
Simba: Ivo Mapunda, Kessy Ramadhani, Mohamed Hussein,Hassani
Isihaka, Juuko Murshid, Abdi Banda/Simon Sserunkuma, Ramadhan Singano, Jonas
Mkude, Ibrahim Ajibu/Elias Maguli, Said Ndemla, Emmanuel Okwi.
Yanga Ally Mustapha, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir
Haroub, Kelvin Yondan, Said Juma, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe,
Mrisho Ngassa/Kpah Sherman,Danny Mrwanda/Hussein Javu.
No comments:
Post a Comment