BONDIA
Mohammed Matumla amewapa raha Watanzania baada ya kumchapa kwa pointi bondia
Wang Xing Hua kutoka China kwenye pambano lililofanyika jana katika Ukumbi wa
Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Matumla ambaye alikuwa akinolewa na baba yake mzazi, Rashid Matumla
'Snake Man' alionyesha kiwango cha juu kwani pambano lilikuwa la vuta nikuvute
hadi akafanikiwa kumshinda Mchina huyo.
Katika
pambano hilo Matumla haikuwa kazi rahisi kwa mtoto huyo wa Matumla kutokana na
kiwango cha juu kilichoonyeshwa na raia huyo wa China kwenye pambano hilo la
raundi kumi
Matumla alifanya kazi kubwa naya ziada kumshinda
Xiang ambaye alionyesha kiwango kizuri hadi kufanikiwa kupata ushindi wa pointi
kwani Mchina
huyo, aliwapa hofu Watanzania waliokuwa ukumbini hapo kutokana na kiwango
kikubwa alichokionyesha.
Hata hivyo
ilipofika raundi ya
nane, baadhi ya Wachina waliokuwa katika ukumbi huo walianza kuondoka wakiamini
ndugu yao asingeshinda pambano hilo.
Katika
pambano lingine la utangulizi bondia Mada Maugo amemaliza
ubishi kwa kumtwanga Japhet Kaseba kwa KO.
Maugo amemchapa Kaseba katika raundi ya nane na kuzima tambo za Kaseba baada ya kumchapa
konde lililompeleka chini na kushindwa kuinuka na mwamuzi akalazimika kumaliza
pambano.
Katika pambano jingine, Karama Nyilawila alimshinda Ibrahim
Tambwe kwa KO katika raundi ya pili na Ashraf
akammaliza Ally Ramadhani kwa KO katika raundi ya pili tu.
No comments:
Post a Comment