Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, March 5, 2015

CRISTIANO RONALDO AIBUKA NA GARI YA MAANA MAZOEZINI


Cristiano Ronald akiwa na Rolls-Royce lake jipya  mazoezini

.MADRID, Hispania
MCHEZAJI Cristiano Ronaldo alirahisisha ufikaji katika mazoezi ya Real Madrid baada ya kutinga na gari lake jipya aina ya Rolls-Royce jeupe lenye thamani ya pauni 330,000 (sawa na Tsh.660,000,000).
Mchezaji huyo bora wa dunia mara tatu aliondoka katika uwanja wa mazoezi kwa staili ya aina yake wakati kocha Carlo Ancelotti akiwaandaa vijana wake kwa ajili ya mchezo wa La Liga dhidi ya Athletic Bilbao utakaofanyika Jumamosi.
Ronaldo alifunga bao lake la 30 la ligi katika mchezo wa mwisho wa Real Madrid dhidi ya Villarreal, lakini haikuwazuia kupoteza pointi mbili baada ya kutoka sare ya 1-1 kwenye uwanja wa Bernabeu.
Zikiwa zimebaki mechi 12 Ronaldo amebakisha bao moja tu kufikisha yale aliyofunga msimu uliopita, na nyota huyo wazamani wa Manchester United amekuwa mchezaji wa kwanza katika historia kutoka katika ligi tano kufunga mabao 30 katika msimu mmoja kwa mara ya tano mfululizo.
Real Madrid iko pointi mbili mbele ya Barcelona kileleni mwa Ligi Kuu ya Hispania huku timu hiyo ikitarajiwa kwenda Nou Camp Machi 22.
Real wanatakiwa kuifunga Bilbao Jumamosi iliyopo katika nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi hiyo kabla hawajaanza kuelekeza nguvu zao katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya siku tatu baadae.
Watakutana na Schalke katika mchezo wa marudiano wa timu 16 bora huku Real Madrid wakiwa na faida ya bao 2-0. Ilikuwa kwenye uwanja wa Veltins Arena huko Ujerumani Februari 18 wakati Ronaldo alipofunga bao la kwanza na kuiweka Real nafasi nzuri ya kufuzu kwa robo fainali.

No comments:

Post a Comment