Haruna Niyonzima na Hamisi Kiiza mashakani michuano ya Kagame |
Akiongea
na mtandao wa LENZI YA MICHEZO, Katibu mkuu wa klabu hiyo Beno Njovu
amesema kocha Maximo bado ameendelea kusisitiza kuwatumia wachezaji
alionao kambini kwasasa wakati huu ambapo wanajiandaa na michuano hiyo
na ligi kuu ya soka Tanzania bara kwani amekwisha kuwafahamu vema akiwa
nao mazoezini.
Njovu
amesema nafasi ya Maximo kwasasa kuwaona wachezaji hao wa kigeni kutoka
Uganda na Rwanda kabla ya michuano ya Kagame Cup kule Rwanda imezidi
kuwa finyu kwasasa kwakuwa wachezaji hao bado wako katika vikosi vya
timu zao za taifa ambazo zitakuwa na majukumu ya kimataifa Agosti 2 na 3
na kwamba muda huo ni mfupi kwao kuweza kurejea Dar es Salaam kwa
maandalizi ya kulekea Kigali.
Rwanda
wanatarajiwa kukutana dhidi ya Congo Agosti 2, wakati Tanzania na
Uganda wakitarajiwa kucheza dhidi ya Msumbiji na Mauritania Ugenini.
Emmanuel Okwi |
Kufuatia
Yanga kuwasajili wachezaji wawili kutoka nchini Brazil msimu
huu Andrey Coutinho na Santos Santana ‘Jaja’ hali imekuwa tete juu ya
hatma ya wachezaji Haruna Niyonzima, Hamisi kiiza Diego na Emmanuel Okwi
ambao mmoja kati yao lazima afutwe ajira yake klabuni hapo, kutokana na
kanuni ya usajili kuibana klabu hiyo ambayo kwasasa inawachezaji sita
huku kanuni hiyo ikitamka klabu kusajili wachezaji watano wa kigeni.
Beno
Njovu amethibitisha kuwa Yanga itaondoka nchini kabla ya Agosti 5 2014
tarehe ambayo si rahisi kwa akina Kiiza, Niyonzima na Okwi hawajatua
nchi kuungana na wenzao kwa safari ya Kigali.
Ingawa
Haruna Niyonzima atapata nafasi ya kuungana na wenzake akiwa Kigali
bado nafasi yake inaonekana kuwa ngumu wakati wa michuano hiyo kwani
Maximo hatakuwa tayari kumtumia kiungo huyo ambaye hakuwahi kuwa naye
hapo kabla.
Yanga
imepangwa katika kundi A pamoja na vilabu vya Rayol ya Rwanda, KMKM ya
Zanzibar, Atlabara ya Sudani kusini na Coffee ya Ethiopia ambapo
wataanza kampeni ya kuwania taji hilo dhidi ya wenyeji Rayol Sports
Agosti 8 uwanja wa Amahoro.
No comments:
Post a Comment