WORLD CUP: BRAZIL 1 vs CHILE 1, WENYEJI BRAZIL WAPETA!! WASHINDA KWA MIKWAJU YA PENATI 3-2! KIPA JULIO CESAR AIOKOA!
WENYEJI Brazil na Chile zilikwenda Dakika 120 huko Estádio Governador Magalhães Pinto, Jijini Belo Horizonte, kwenye Mechi ya Raundi ya Pili ya Fainali za Kombe la Dunia baada kutoka Sare 1-1 katika Dakika 90 na pia kumalizika hiyo nyongeza ya Dakika 30 bila Mshindi na hatimae Brazil kupita kwa Mikwaju ya Penati 3-2 huku Kipa wao Julio Cesar akiibuka Shujaa kwa kuokoa Penati 2 kati ya hizo.
Brazil walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 18 la David Luiz alieunganisha Mpira uliopigwa Kona na Neymar na kugongwa na Thiago Silva.
Kipindi cha Pili Hulk aliifungia Brazil Bao la Pili lakini Msaidizi wa Refa Howard Webb kutoka England aliashiria Mbrazil huyo alishika kabla kufunga.
Hadi Dakika 90 kumalizika Bao zilikuwa 1-1 na Nyongeza ya Dakika 30 haikuzaa Mshindi na Mechi kuingia Tombola ya Mikwaju ya Penati ambazo Brazil walishinda kwa Penati 3-2 na kutinga Robo Fainali ambapo watakutana na Mshindi kati ya Colombia na Uruguay wanaocheza baadae leo.
Alexis Sanchez akishangilia bao alke la kusawazisha katika dakika ya 32
Mchezaji anayekipiga katika Klabu ya Barcelona Alexis Sanchez ndie aliyewasawazishia bao Chile na kufanya 1-1 dhidi ya Brazil katika dakika ya 32 kipindi cha kwanza.
Bao...
Mashabiki wa Chile
Thiago Silva na mchezaji wa Chile Mauricio Pinilla wakiombana yaishe na kutakiana heri kipute kiendelee baada ya kukwatuana chini. wakikubaliana kwamba majambo kama yapo ya kawaida kwenye soka!!
Wachezaji wa Brazil wakipongezana walipopata bao lao kwenye dakika za kipindi cha kwanza.
Brazil: Julio Cesar, Dani Alves, Thiago Silva, Luiz, Marcelo, Fernandinho, Gustavo, Hulk, Oscar, Neymar, Fred.
Subs: Jefferson, Paulinho, Dante, Maxwell, Henrique, Ramires, Hernanes, Willian, Bernard, Jo, Maicon, Victor.
Chile: Bravo, Mena, Isla, Silva, Alexis, Vidal, Vargas, Medel, Jara, Aranguiz, Diaz.
Subs: Toselli, Albornoz, Carmona, Pinilla, Valdivia, Rojas, Orellana, Beausejour, Gutierrez, Fuenzalida, Paredes, Herrera.
Referee: Howard Webb (England)
Post a Comment