Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, February 11, 2014

WATANO KANEMBWA JKT WAFUNGIWA MECHI TATU

Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imewafungia mechi tatu wachezaji watano kati ya tisa wa timu ya Kanembwa JKT waliolalamikiwa na Sekretarieti kwa kumpiga mwamuzi kwenye mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) iliyochezwa Novemba 2 mwaka jana.

Wachezaji hao ni Bariki Abdul, Mrisho Musa, Nkuba Clement, Nteze Raymond na Philo Ndonde. Wachezaji ambao hawakutiwa hatiani kutokana na ushahidi dhidi yao kutojitosheleza ni Abdallah Mgonja, Mbeke Mbeke, Ntilakigwa Hussein na Uhuru Mwambungu.

Mechi hiyo dhidi ya Stand United iliyochezwa Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga ilivunjwa na refa Peter Mujaya dakika ya 87 kutokana na kupigwa na wachezaji hao baada ya kuamuru ipigwe penalti dhidi ya timu yao.

Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Ibara ya 49 (1)(b) ya Kanuni za Nidhamu za TFF baada ya kupitia vielelezo vilivyowasilishwa na Sekretarieti ya TFF ambavyo ni ripoti ya refa, ripoti ya kamishna wa mechi hiyo na video iliyoonesha tukio hilo.

Pia kabla ya kutoa adhabu baada ya kusikiliza utetezi kutoka kwa walalamikiwa ambao ni wachezaji hao na timu yenyewe ya Kanembwa JKT. Nayo Kanembwa JKT imetiwa hatiani na kupigwa faini ya sh. milioni ambayo inatakiwa kuilipa kabla ya kucheza mechi inayofuata.

Kamati hiyo iliyokutana Februari 9 mwaka huu chini ya Mwenyekiti wake Tarimba Abbas, kwanza imelaani kitendo cha wachezaji wa timu hiyo kumzonga refa, kwani vitendo vya aina hiyo ndiyo vichocheo vya vurugu viwanjani.

Lakini pia imempongeza nahodha wa Kanembwa JKT, Mbeke Mbeke kwa kuwa mstari wa mbele kuwazuia wachezaji wenzake waliokuwa wakimpiga refa wa mchezo huo.

Vilevile Kamati hiyo imesema aliyesababisha matatizo hayo ni refa Mujaya, na ingawa ilikuwa na uwezo wa kumchukulia hatua lakini haikufanya hivyo kwa vile hakukuwa na mlalamikaji na tayari Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ilishamwadhibu.

No comments:

Post a Comment