KIONGOZI wa
bendi ya Musica Creation, Rissa Risasy
amewataka wapenzi wa muziki wa dansi kujiandaa kupata burudani halisi ya muziki
wa dansi yenye vionjo vya kiafrika.
Risasy
aliyasema hayo wakati alipozungumza na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa
bendi hiyo utakaofanyika siku ya Wapendanao katika Ukumbi wa Cassa Complex,
uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Mwanamuziki
huyu mkongwe kwenye muziki wa dansi alisema kuwa bendi hiyo inamilikiwa na
familia yake na itakuwa ikitoa burudani hapa nyumbani na nje ya nchi kwani
watakuwa wakisafiri kufanya maonyesho.
Bendi hiyo
inapiga kwa kutumia ‘Sofiyanika’ na ina vyombo vyenye uwezo wa kurekodi wakati
wakimba ina wanamuziki nane, watano wakiwa wazawa wa Tanzania na watatu
wanatoka nje ya nchi na ina albamu mbili.
Pia alisema kiingilio kwenye uzinduzi huo ni 30,000
kwa VIP, 15,000 na 10,000 na burudani itaanza saa 3:00 hadi majogoo.
Rissa Risasy
aliingia Tanzania mwaka 1987 baada ya kufuatwa DRC na mke wa Lovy Longomba
kuanzisha bendi ya Afriso Ngoma, baadae alihamia Sambulumaa bandi kisha Maquis
na kuchukuliwa Virunga ya Kenya.
No comments:
Post a Comment