Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, February 13, 2014

COPA DEL REY: FAINALI SASA NI ‘EL CLASICO’ KATI YA REAL MADRID vs BARCELONA

BARCELONA Jana Usiku wameitengeneza ‘El Clasico’ ambapo watakutana na Watani zao Real Madrid kwenye Fainali ya Kombe la Mfalme, Copa del Rey, baada kutoka Sare ya Bao 1-1 na Real Sociedad kwenye Estadio Anoeta na kusonga kwa Jumla ya Bao 3-1.
Katika Mechi ya Kwanza huko Nou Camp Wiki iliyopita, Barca iliichapa Real Sociedad Bao 2-0.


Kwenye Mechi ya Jana Usiku, Barca walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 27 la Lionel Messi na Real Sociedad kusawazisha katika Dakika ya 87 kwa Bao la Antoine Griezmann.

Juzi, kwenye Marudiano ya Nusu Fainali nyingine ya Kombe hili, Bao mbili za Cristiano Ronaldo ziliwabwaga nje waliokuwa Mabingwa Watetezi wa Kombe hili, Atletico Madrid, waliofungwa 2-0 na Real Madrid na kutolewa kwa Jumla ya Bao 5-0 kwani walichapwa 3-0 huko Santiago Bernabeu katika Mechi ya Kwanza Wiki iliyopita.

Fainali itachezwa hapo Aprili 19 katika Uwanja utakaotangazwa baadae.
COPA del REY
NUSU FAINALI/MATOKEO
Marudiano
Jumanne Februari 11

Atletico de Madrid 0 v Real Madrid CF 2 [0-5]
Jumatano Februari 12
Real Sociedad 1 v FC Barcelona 1 [1-3]

FAINALI
Aprili 19

Real Madrid v Barcelona

No comments:

Post a Comment