Wakuu wa Vyombo vya Habari
TANZANIA.
Kambi ya
Tanzania Top Models iliyoanza 7.11.2013 katika Hotel ya JB Belmont inaendelea
vizuri ikiwashirikisha washiriki 16 badala ya 20 waliokuwa wamechaguliwa
kujiunga na kambi hii. Wasichana walioshindwa kujiunga na kambi kwa sababu
mbali mbali hasa kutokana na shule au kukataliwa na wazazi ni Esther Albert wa
Dar es salaam, Jackline Kimambo wa Dodoma, Neema Selei wa Arusha na Esther
Frederick wa Moshi. “Tunamshukuru Mungu leo ni siku ya 14 wasichana wakiwa
kambini” na mambo yakiendelea vizuri ingawa kumekuwepo na changamoto kadhaa
kama kuugua kwa baadhi ya Models na mapungufu ya vitu vidogo vidogo kutokana na
kutokuwepo wadhamini wa kutosheleza mahitaji yote. Kambi yetu ilihama katika
Hotel JB Belmont na kuhamia hapa tulipo kwenye Hotel Tamal siku ya Jumatatu
18.11.2013 na tunaendelea vizuri na mazoezi yetu, washiriki wetu wakiwa katika
hali nzuri na wenye hamasa ya kushindana hapo ifikapo 7.12.2013.
Mashindano
yetu ambayo yatakuwa sehemu ya shamrashamra za kusheherekea miaka 52 ya uhuru
wa Tanzania Bara, yatahusisha washiriki kuvaa na kuonyesha mavazi ya aina nne.
Mavazi hayo yatakuwa ni Vazi la kitanzania(Tanzanian Dress), vazi la kubalizi
(Cocktail Dress), Vazi la kiofisi(Office Dress) na Vazi la Jioni Evening Dress.
Pamoja na Wanamitindo hawa kushindana katika mavazi, pia watashindana katika
vipaji hadi tupate mshindi ambaye atatuwakilisha katika mashindano ya Top Model
of the World yatakayo fanyika mwezi wa March 2014. Tunaendelea kujiandaa na
shindano hili kwa washiriki kufanya mazoezi ya kutosha na kwa waandaji
kuendelea kutafuta wadhamini na kutimiza wajibu wetu ili shindano letu liwe
zuri na la kuvutia. Mazoezi yanayoendelea kwenye kambi yanaendeshwa na waalim
sita. Zakia Twahir anafundisha kutembea (catwalk), Badspencer anafundisha na
kuendeleza vipaji vya uchezaji wa muziki wa dance, Wanne Salim anafundisha na
kuendeleza vipaji vya uchezaji wa ngoma na utamaduni, Dokta Cheni na Shuzi
wanafundisha na kuendeleza vipaji vya kuigiza, ambapo ….. anafundisha na
kuiendeleza vipaji vya kuimba.
Ni vyema tutumie nafasi hii leo kuzindua upigaji wa kura kwa
washiriki wetu. Tunaomba wananchi waanze kufuatilia shughuli za washiriki leo
usiku katika vituo vya Luninga vya Clouds TV na Tumaini TV ili waone kinachoendelea
kwenye kambi na kupiga kura kwa mshiriki anaye kuvutia. Tunahimiza wananchi
kupiga kura mara nyingi iwezekanavyo ili kumfanya mshiriki anayependwa na
kupata kura nyingi aweze kushinda. Unachotakiwa kufanya wakati wa kupiga kura
ni kutuma ujumbe kwa simu ya mkononi kwenda kwenye Namba 15564 ukiandika
TM(unaacha nafasi) halafu jina la mshiriki unayempenda. Mfano unaandika “TM
Jackline” na kutuma kwenda 15564. Majina ya Models wanaoshiriki na ambao
wanaomba kura ni
·
AMMARA . DARLINE . EVE .
GAUDENCIA
·
IRYNA . LORRAINE . MATUREGE .
MIRACLE
·
NAIMA . NEMIC . NILER . NURU
·
RETTY . GLADYS . TINA . ZULPHER
Tunaomba wananchi watuunge mkono kwa kuendelea kupiga kura
na kufanya mchuano wa kumtafuta Tanzania Top Model kuwa wa mafanikio na wenye
tija. Mshiriki atakaye pata kura nyingi atajinyakulia Taji la Princess of
Tanzania na kupata alama nyingi zitakazo mwezesha kushinda na kuwa Tanzania Top
Model. Mataji mengine yatatolewa kwa Mwanamitindo atakaye pendeza zaidi katika
vazi la kitanzania(best in Tanzanian Dress) pamoja na Tuzo kwa Mwanamitindo
mwenye muonekano mzuri kwenye picha(Photogenic award). Mbunifu wa mavazi
atakayekuwa amemvalisha Mshiriki atakayeshinda katika vazi la Kitanzania
atapewa Tuzo kama Mbunifu bora wa vazi la kitanzania kwa mwaka 2013.
Ili kufanikisha shindano hili, tunao washirika ambao wako
bega kwa bega na Kampuni yetu ya Tanzania Top Model Agency Limited,tunawashukuru
sana.
1.
Data
vision International - Mshirika wetu katika teknologia(Technology Ptner)
2.
Haakneel
Production – Mshirika wetu kwenye uzalishaji (Production Partner)
3.
Giraffe
Ocean View Hotel – Mshirika wetu kwenye Ukarimu (Hospitality Ptner)
4.
Clouds
Media Group – Mshirika wetu wa Utangazaji.(Media Partner)
Pia tunao wadhamini mbalimbali ambao wametusaidia na wako tayari
kufanikisha shindano hili. Tunawashukuru sana JB Belmont Hotel, For you
Boutique, Shear Illusion, NSSF, Tamal Hotel, Screen Masters, TV Tumaini, Man
Magazine, Fabak Fashion, TV Africa na Rio Gymn. Nafasi za kudhamini bado zipo
na tunatoa mwito kwa wale wenye maono ya baadaye wajitokeze waje kutudhamini sasa
ili tuweze kukua pamoja.
Tunashukuru vyombo vya habari vyote na hasa nyinyi mlioko
hapa ambao mmekuwa mkifanya shindano la Tanzania Top Model kuwa katika masikio
ya watanzania wengi na kulifanya liwe maarufu sana tangu kuzinduliwa kwake
kinyume na tulivyotarajia.
Asanteni.
Jackson
M.Kalikumtima
Mwenyekiti
Mtendaji
Tanzania
Top Model Agency Ltd
No comments:
Post a Comment