UEFA CHAMPIONS LEAGUE: BORUSSIA DORTMUND vs ARSENAL, CHELSEA vs SCHALKE 04, ARSENAL UGENINI...CHELSEA NYUMBANI DARAJANI
Klabu za England, Chelsea na Arsenal, kupambana leo na wapinzani kutoka Bundesliga huko Germany. Chelsea watacheza kwao Stamford Bridge na FC Schlake 04, Timu ambayo waliicharaza bao 3-0 huko Veltins Arena, Mjini Gelsenkirchen, Germany hapo Oktoba 22, na Arsenal wako Ugenini kurudiana na Borussia Dortmund ambayo iliipiga Arsenal 2-1 Uwanjani Emirates hapo Oktoba 22.
Arsenal wako Kundi F ambalo Vinara ni Borussia Dortmund wakifuatia Arsenal kisha Napoli lakini Timu zote hizi zina Pointi 6 kila mmoja na Marseille yuko mkiani akiwa hana hata Pointi.
Arsenal wanatinga kwenye Mechi na Borussia Dortmund wakiwa ni Vinara wa Ligi Kuu England kwa Pointi 5 mbele baada ya hivi Juzi kuifunga Liverpool Bao 2-0.
Chelsea wako Kundi E wakiongoza na Pointi 6 sawa na Schlake na Nafasi ya Tatu ni FC Basel wenye Pointi 4 na mkiani ni Steau Bucharest wenye Pointi moja tu.
Chelsea wanacheza na Schalke huku wakitoka kwenye kipigo kwenye Ligi Kuu England baada ya Jumamosi kupigwa 2-0 na Newcastle kitu ambacho kimemkasirisha Meneja wa Jose Mourinho ambae amewaonya Wachezaji wake kuacha uzembe na pia kudaiwa kumpigwa kwanja Beki wa Brazil David Luiz.
Mechi nyingine kubwa ni huko Nou Camp Mjini Barcelona Nchini Spain ambako Mabingwa wa Spain, FC Barcelona, watakaporudiana na AC Milan ambao walitoka nao 1-1 Wiki mbili zilizopita.
Barcelona, ambao wamepoteza Pointi 2 baada kwenda Sare ya Bao 1-1 na AC Milan kwenye Kundi H, wanaweza kufuzu ikiwa wataifunga AC Milan Uwanjani Nou Camp hapo Jumatano na matokeo mengine kwenye Kundi kuwa mazuri kwao.
FC Basel 1893 v FC Steaua BucureÅŸti
Chelsea FC v FC Schalke 04
Borussia Dortmund v Arsenal FC
SSC Napoli v Olympique de Marseille
Football Club Zenit v FC Porto [Saa 2 Usiku]
Club Atlético de Madrid v FK Austria Wien
AFC Ajax v Celtic FC
FC Barcelona v AC Milan
Post a Comment