IMU ya Taifa, "Taifa Stars" sasa inacheza na Zimbabwe mechi ya
Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)- utakaochezwa Jumanne Novemba 19 mwaka huu Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam.
Awali Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager
ilikuwa icheze na Kenya (Harambee Stars), lakini Shirikisho la Mpira wa Miguu
Kenya (FKF) lilituma taarifa jana jioni (Novemba 16 mwaka huu) likieleza kuwa
timu yake haitacheza tena mechi hiyo.
Kikosi cha Zimbabwe chenye msafara wa watu 30 kinatarajia
kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kesho (saa 3
asubuhi) tayari kwa mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 11 kamili jioni.
Waamuzi wa mechi hiyo wanatoka Uganda wakati Kamishna atakuwa
Leslie Liunda wa Dar es Salaam. Mwamuzi wa mezani ni Oden Mbaga pia wa Dar es
Salaam.
Stars chini ya Kocha Kim Poulsen ipo kambini tangu Novemba 12
mwaka huu kujiwinda kwa mechi hiyo. Kim amejumuisha kwenye kikosi chake wachezaji
watano wanaocheza mpira wa miguu nje ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment