|
Kamisaa wa mchezo, Joseph Kanakamfumu akimpokea Makamu wa Rais wa TFF Wales Karia na viongozi mbali mbali kwa ajili ya kusalimiana na wachezaji |
|
Makamu wa Rais wa TFF Wales Karia akisalimiana na waamuzi |
|
Makamu wa Rais wa TFF Wales Karia akisalimiana na wachezaji wa Azam FC |
|
Makamu wa Rais wa TFF Wales Karia akisalimiana na wachezaji wa Coastal Union |
|
Makamu wa Rais wa TFF Wales Karia akisema neno kuashiria ufunguzi wa mashindano |
|
Waamuzi na timu wanapiga kura kuchagua timu ya kuanza mchezo |
|
Benchi la Azam FC |
|
Benchi la Coastal Union |
|
Viongozi wakifuatilia mpambano |
|
Wachezaji wa Azam FC wakishangilia bao |
|
Wachezaji wa Coastal Union |
|
"Unipiti kirahisi wewe" |
|
Kocha wa Coastal Union Mkenya Yusuph Chiko
|
TIMU ya Azam Fc inayoshiriki michuano ya vijana wenye umri wa chini ya
miaka 20 (U20) kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom leo imeanza vibaya mashindano
hayo baada ya kufungwa mabao 2-1 na Coastal Union ya Tanga.
Azam ambao walikuwa wa kwanza kupata bao kwenye
dakika ya tatu kupitia kwa mshambuliaji Eric Haule baada ya kuwazidi mbio
mabeki wa Coastal Union, bao ambalo lilidimu kwa kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu kufanya
mabadiliko, hali iliyofanya mchezo kubadilika na kushambuliana kwa zamu lakini
zamu hii Coastal waliizidi Azam Fc kila sehemu.
Iliichukua Coastal Union dakika tano (daakika ya
50) kwenye kipindi cha pili kusawazisha bao kupitia kwa kiungo mshambuliaji
Raizin Haji kwa njia ya penati baada ya beki wa Azam Fc kunawa mpira eneo la
hatari.
Dakika tano baadae (dakika ya 55) Raizin Haji
aliifungia Coastal bao la pili baada ya kuwapiga chenga mabeki wa Azam hadi
golikipa na kutia mpira wavuni kirahisi na kuamsha nderemo na vifigo kwa
mashabiki waliokuwa wamefurika uwanjani hapo.
Baada ya matokeo hayo Azam walionekana kuchoka
na kushindwa kuhimili mashambulizi ya Coastal lakini shukrani kwa mlinda mlango
wao Hamadi Juma kwani alijitahidi kuokoa michomo mingi licha ya kufungwa hayo
mabao mawili.
Awali akifungua mashindano hayo Makamu wa Rais
wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF) Wales Karia alishukuru udhamini wa maji ya
Uhai kwani umesaidia kuibua vipaji na kusema TFF ina mikakati ya kuongeza
mashindano mengi ya kuhusisha umri ukiacha yale ya U-15 yanayodhaminiwa na Coca
cola.
“Nashukuru udhamini wa maji ya Uhai kwani vijana
wanatakiwa wacheze mara kwa mara ili kusaidia kuinua vipaji ambavyo vitakuwa
hazina kwa taifa hapo baadae”, alisema Karia.
No comments:
Post a Comment