Mjane wa Daudi Mwangosi Itika Mwangosi kulia akifuatilia matukio yanayoendelea katika ukumbi huo |
Meneja wa uthibiti wa ubora kutoka baraza la habari Tanzania (MCT) Pili Mtambalike ametoa kauli hiyo leo jijini Mwanza wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo ya kishujaa na uandishi uliotukuka ya Daudi Mwangosi .WANAHABARI nchini wametakiwa kujenga umoja katika kupinga sheria kandamizi ya vyombo vya habari na wanahabari nchini inayatarajia kupitishwa na wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Mtambalike amesema kuwa idadi ya waandishi kutekwa na kuuwawa imezidi kuongezeka hapa nchini huku kasi ya serikali kuvifungia vyombo vya habari pia inaendelea kuongezeka .
Hivyo iwapo wanahabari nchini hawataungana katika kupinga manyanyaso dhidi ya vyombo vya habari na kupinga sheria kandamizi dhidi ya vyombo vya habari na wanahabari suala la uhuru wa vyombo vya habari nchini litaendelea kubaki ndoto.
Kwa upande wake rais wa umoja wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Keneth Simbaya alisema kuwa tuzo hiyo inayotolewa ni tuzo ya kwanza kutolewa nchini Tanzania kwa waandishi wanaopata matatizo wakati wanatekeleza wajibu wao.
Simbaya alisema kuwa UTPC imeamua kuanzisha tuzo hiyo kama njia ya kuwapa moyo wanahabari na kuuthibitishia umma kuwa wanahabari nchini hawatakata tama katika kutumikia tasnia hiyo.
Alisema iwapo jamii inapaswa kujua ni vema serikali kukubali kutoa habari kwa jamii inayopasa kujua na inayo haki ya kupata habari.
“ Serikali itambue kuwa inapohitaji wananchi kuchangia maendeleo ni vema itambue kuwa wananchi hao wana haki ya kupata taarifa mbali mbali ya kile walichochangia….ndani ya tukio la mauwaji ya Mwangosi tumejifunza mambo mengi sana kwani tunapofanya kazi zetu wapo wasiopenda kuona tunafanya kazi zetu hiyo”
Pia alisema ni vizuri wananchi kutambua kuwa wakati wanahabari nchini wakitetea kupata habari wasifikiri wanahabari wanajipangani wao .
Kwani alisema kuwa jitihada za wanahabari kupigania uhuru wa kupata habari zinapaswa kuungwa mkono na kila raia wa Tanzania ambayo ana haki ya kupata habari
Jaji mkuu tuzo hiyo Hamza Kasongo alisema kuwa mchakato wa kumpata mshindi ulifanyika kwa kipindi cha miezi miwili kuanza septemba hadi Octoba mwaka huu.
Tuzo hiyo ya uandishi wa habari wa kishujaa na utumishi uliotukuka ya Daudi Mwangosi imetolewa kwa Absalom Kibanda mahariri wa kampuni ya new habari (2006) Ltd na mwenyekiti wa jukwaa la wahariri nchini (TEF).
No comments:
Post a Comment