MADRID, Hispania
UTAMU. Pasi nyingi. Wanatawala mchezo dakika zote 90. Hawapangi namba
tisa mbele ya lango la adui. Cesc Fabregas ndiye alitolewa mhanga kucheza namba
tisa. Wakati wa kombe la mataifa ya Ulaya mwaka 2008, Fernando Torres alishirikiana
na David Villa katika safu ya ushambuliaji.
Lakini kwenye kombe la dunia mwaka 2010 wote waliwekwa kando. Kwenye
kombe la mataifa ya ulaya mwaka 2012 hali ikawa ileile. Sasa mambo
yamebadilika. Ni mwisho wa Armada. Anzia Fernando Torres, halafu angalia kwenye benchi
wapo Roberto Soldado na Alvaro Negredo, kasha David Villa akibaki chaguo la
tatu.
Hispania ilitengeneza
namba tisa feki, lakini sasa inaonekana kuachana amarda. Ukiambiwa amarda ni ni
aina ya uchezaji ambao Hispania iliuingiza kwenye soka. Wakicheza hawamtaki
namba tisa, na Torres akawa mchezaji wa kawaida kuliko umuhimu wake.
Ndani ya 18 Hispania
walihitaji kiungo mshambuliaji ambaye atasaidia kuifanya timu iendelee kupiga
pasi, si kuwa na mshambuliaji ambaye wanaona anaharibu staili yao. Wakicheza
Tiki-Taka, wanazunguka kila kona, mabeki wa kulia na kushoto wanaigia staili ya
Brazil, yaani wanachezwa kama mawinga.
Hispania haikuhitaji
mshambuliaji kamili, lakini sasa mam,bo yamebadilika na staili yao ya Amarda
inaonekana kufa kabisa. Pep Guardiola alimuuza Samuel Eto’o kwenda Inter Milan
na kumleta Zlatan Ibrahimovic, lakini kwa staili yao ya Amarda wakahindwa
kumtumia. Wakaona Zlatan anaharibu mfumo wao, wakimtupia virago.
Lakini leo hii Pep
Guardiola akiwa na Bayern Munich anatumia mbinu zote mbili; kwanza akitumia
amarda anamuondoa Mario Mandzukic, na kumpanga Thomas Muller nafasi ya
ushambuliaji, kasha Toni Kroos anakuwa nyuma yake, pili baadhi ya mechi
anavunja amarda na kumpanga Mario Mandzukic, kwa mfano mechi ya Supercup.
Lakini sasa mambo
yamebadilika kwa kasi sana Pep Guardiola anamkaribisha mshambuliaji hatari wa
Borussia Dortmund, Robert Lewandowski kuanzia msimu ujao. Bayern wameshamchukua
Lewandowski ikiwa na maana watampanga mshambuliaji kamili badala ya amarda
inayotumiwa na Guardiola.
UUCHEZAJI
WA AMARDA 4-6-0
Pengine baadhi ya mashabiki
watashangaa kusikia jina la amarda. Lakini mfumo wake unapangwa kwa mabeki
wanne, viungo sita na safu ushambuliaji hakuna mchezaji anayecheza. Hii ina maana ni 4-6-0 ambayo inatukumbusha zama za Hector Cuper alipoifundisha Inter Milan mwanzoni mwa miaka 2000 alitumia mfumo wa 9-1. Afadhali yeye alipanga 9-1 akiwa na mshambuliaji mmoja mbele, lakini 4-6-0 haimtaki mshambuliaji yeyote.
Mwaka 2007 aliyekuwa kocha wa AS Roma, Luciano Spaletti alikuwa akimtumia Francessco Totti katika mfumo wa amarda, 4-6-0. Tangu wakati huo, wengi waligundua kuwa kocha huyo alichukua mfumo wa Barcelona, ambapo kocha Pep Guardiola alipendelea kumpanga Lionel Messi katika ushambuliaji.
Huu ni urithi wa Guardiola aliouacha Barcelona na kumsaidia kutwaa mataji mbalimbali ndani ya Hispania mpaka Ulaya.
UTUNDU WA MARCELO BIESLA
Wakati mbunifu wa amarda, Johan Cruyff, aliwatumia wachezaji wa kawaida, Guardiola alimtumia mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu na bingwa wa soka la kisasa na Tiki-taka. Messi alimudu amarda, aliburudisha kama mtangulizi wake Ronaldinho Gaucho.
Lakini Cruyff alitegemea 4-6-0, lakini Pep Guardiola akaongeza kitu kingine alichochukua kwa Marcelo Biesla raia wa Argentina na mkali wa mfumo wa 4-3-3. Pep aliona mfumo wa 4-3-3 unaweza kupambana na timu zinazojihami na kushambuliaji kwa kushtukiza.
Akampanga Sergio Busquets kama kiungo wa ulinzi, Messi alicheza kwa uhuru mbele ya lango la adui. Messi hakulazimika kupambana na mabeki wa timu pinzani. Lakini Pep akaona haitoshi, akatengeneza viungo wengi katikati ya dimba, akaubadili mfumo wa Biesla, na kutumia 3-4-3.
Kwahiyo akawa na mifumo mitatu 4-6-0, 4-3-3 na 3-4-3 kutegemeana na mechi. Wakati Guardiola akiwa Barca alitumia wachezaji watatu katika staili ya amarda, kati ya Lionel Messi, Andres Iniesta na Xavid Hernandez.
Wote walitakiwa kupiga pasi, kutawala mchezo dakika zote na kufunga mabao katika mfumo wa pembetatu. Ndio maana Thiery Henry na Samuel Eto’o akalazimika kucheza pembeni na kumwachia Messi kama namba tisa feki.
TATA MARTINO
Barca ni ileile licha ya kuwa na kocha mpya, Gerardo ‘Tata’ Martino, ambapo safu ya ushambuliaji inao Neymar Junior, Alexis Sanchez, na Pedro Rodriguez. Lakini mchezaji ambaye anakamilisha amarda ni Lionel Messi, wengine wote wanachezwa pembeni kumpisha yeye.
Pedro anacheza pembeni kama Neymar na Alexis, hii ikiwa na maana eneo la namba tisa halina mtu, kwani Messi anacheza nyuma ya eneo la hatari. Hii ndio amarda.
VICENTE DEL BOSQUE
Kocha wa timu ya taifa ya Hispania Vicente Del Bosque anaonekana kubadilika sasa tangu kumalizika kwa mashindano ya kombe la mabara. Del Bosque alitumia Cesc Fabregas, lakini sasa anawapa nafasi Roberto Soldado na Alvaro Negredo, huku David Villa na Torres wakitegemewa kuanzia benchi.
Kuna Fernando Llorente, na mshambuliaji anayekuja juu Alvaro Morata. Ni wazi amarda imefika mwisho, lakini safu ya kiungo itawategemea Sergio Busques na Xabi Alonso, huku mawinga halisi Jesus Navas na Pedro Rodriguez wanategemewa kucheza pia.
No comments:
Post a Comment