Unajua nini Manchester United
inatakiwa kufanya kwa sasa? Ni kufungua pochi tu, kuongeza dau la pauni milioni
30 walilolitoa kwa klabu ya Athletic Bilbao ya kwa ajili ya kiungo muhispani
Ander Herrera, mwishoni mwa wiki hii na kukataliwa.
Pengine hili ndo suluhisho la kocha wa
mashetani hao wa kutoka katika jiji la Manchester katika nafasi ya kiungo ambayo
imekuwa ikususua sua kwa kipindi kirefu.
Moyes alikuwa kocha wa Evarton kwa
msimu uliopita kabla ya |Sir Alex Furgson kupendekeza jina lake kama mrithi wa
kiti chake kutokana nay eye kutangaza rasmi kustaafu soka na kusalia kama
mshauri wa klabu na kuendelea kuwa balozi wa klabu katika masuala mabalimbali.
Moyes alikuwa na nia ya kuondoka na
kiungo wa Ervaton Maroune
Fellain kumaliza tatizo la mabingwa hao wa England kwa msimu
uliopita lakini klabu ya Ervaton imezitupilia mbali mara mbili ofa
zilizopelekwa na Manchestera suala ambalo linaonyesha dhairi kuwa hawapo tayari
kumwachia kiungo huyo.
Ni
dhairi shairi kuwa Manchester imekuwa na tatizo la kiungo kwa muda mrefu tangu
alipotangaza kuachana na soka kiungo machachari Paul Scholes.
Scholes
ndiye alikuwa msaada mkubwa wa Manchester United kwa kipindi cha muda mrefu na
ameendelea kuwa moja ya viungo wachezeshaji bora barani Ulaya na duniani kwa
ujumla.
Manchester
wanajua umuhimu wa Scholes na Furguson anajua kuwa kiungo huyo aliandaliwa kwa muda mrefu na ilikuwa
kazi ngumu kwa klabu hiyo kupata mridhi wake ndiyo maana baada ya kustaafu
waliamua kumrudisha japo kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Tangu
enzi za Furgason Manchester im ekuwa ikisaka kiungo imekuwa ikitupa karata zake
kwenye majina mbalimbali makubwa katika vipindi mbalimbali vya usajili,
akuiwemo Wesley Sneidjer wakati akiwa Inter Milan.
Vita
hii imeendelea kwa kujaribu kunasa majina mbalimbali akiwemo Fellain mwenyewe,
kiungo wa Barcelona
Cesc"
Fàbregas ambaye klabu yake nayo haikuwa tayari kumuachia na kiungo
mwingine wa klabu hiyo ya wakatalunya Thiago Alcântara ambaye yeye aliamua
kumfuata kocha wake wa zamani Pep Guardiola anayewanoa miamba wa
Ujerumani(Bunder Sliga) Bayern Munich.
Jaribio
linguine sasa Moyes anafanya kwa kiungo wa kimataifa wa mabingwa wa dunia
Hispania katika timu ya vijana chini ya miaka 19, 20 na chini ya miaka 21 na
sasa katika timu ya wakubwa.
Moyes
amepelekana ofa ya pauni milioni 30 kwa ajili ya kiungo wa zamani wa timu ya
Hispani ya chini ya miaka 21(U-21) Ander Herrera lakini klabu yake ya
Artiletico Bilibao imetupilia mbalia ofa hiyo.
Mwenyekiti
wa klabnu hiyo Josu UrrutI aliwambia waandishi wa habari juzi Ijumaa kuwa
wamepokea ofa kutoa Manchester United
lakini wameikataa kwa kuwa lengo la klabu hiyo siyo kufanya biashara ya
wachezaji bali kutengeneza kikosi imara.
“Kuna
ofa kutoka Manchester United kwa ajili ya Ander Herrera," Urrutia aliwambia waandishi. "Klabu yetu ni
tofauti sana na klabu nyingine mnazozifahamu, inajitegemea yenyewe. Lengo letu
si kutengeneza pesa, tunaiona Athletic a
kama klabu ya kipekee na wachezaji wanatakiwa kutambua hivyo.
"Hili mchezaji aondoke hapa anatakiwa
kuonyesha nia kuwa anataka kuondoka na anatakiwa kutuambia ndiyo tuanze
kukubalia ofa zinaz." Aliongeza.
Kazi
iliyosalia kwa United ni kuongeza pesa kwa ajili ya kuishawishi klabu hiyo
kumuachia mchezaji huyo kama ambovyo klaby ya Beryen Munich ilivyofanya kwa kwa
kutoa Pauni milioni 40 kwa ajili ya Javi Martinez ambaye kwa sasa amnaitumikia
timu hiyo ya Ujerumani.
No comments:
Post a Comment