KIINGILIO MECHI YA SIMBA, YANGA 5,000/- MPAKA 30,000/-
Kiingilio si tatizo tunataka kuingia kumuona Mnyama!!
Yanga wakifurrahia moja ya ushindi wao -TaifaKiingilio cha chini kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Yanga itakayochezwa Jumapili (Octoba 20 mwaka huu) kitakuwa sh. 5,000. Kiingilio hicho ni kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648.
Tiketi zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya
mchezo huo utakaoanza saa 10 kamili jioni katika vituo mbalimbali. Vituo
hivyo ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa
Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta
Buguruni, Dar Live Mbagala,
Uwanja wa Uhuru, na BMM Salon iliyoko Sinza
Madukani. Mechi hiyo namba 63 itachezeshwa na Israel Nkongo kutoka Dar
es Salaam, ambapo atasaidiwa na Hamis Changwalu wa Dar es Salaam pia, na
Ferdinand Chacha wa Bukoba. Mwamuzi wa akiba ni Oden Mbaga wa Dar es
Salaam. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa John Kiteve kutoka Iringa wakati
mtathmini wa waamuzi (referees assessor) ni Stanley Lugenge wa Njombe.
Post a Comment