MUNICH, Ujerumani
SI soka tu. Si chenga za Robben. Si
hamasa na ufundi wa Pep Guardiola. Si kasi ya Frank Ribery. Si kukaba kwa
Philip Lahm au Rafinha. Lakini Bayern Munich wanajua namna ya kula bata.
Unajua kilichotokea? Pep Guardiola amekuwa
mmoja wa watu walioonja raha ya kuifundisha Bayern Munich.
Kila timu inakuwa na utamaduni wake.
Brazil wanapenda sherehe za Samba, lakini Bayern Munich wao wanayo Oktoberfest
ambayo inakuwa full bata kila mwaka.
Munich ni mabingwa wa Ulaya.
Wanakunywa na kulewa, wanaburudika kwa kila namna, huo ndio utamaduni wao na
kutangaza siku yao ya mwaka, Oktoberfest.
Oktoberfest ni siku ya kifamilia
katika timu ya Bayern Munich. Ni sherehe za kila mwaka kama ambavyo hapa Tanzania
inavyofanyika Fiesta katika mikoa mbalimbali.
Kocha huyo wa zamani wa Barcelona,
alionja utamu wa kuifundisha timu hiyo pale alipolazimika kuvaa mavazi ya
kiutamaduni, yeye na mkewe pamoja na wachezaji wote wa Bayern Munich.
Sherehe hizo zinawaunganisha
wachezaji, viongozi, wenyeji na wageni maalumu wanaoalikwa kuhudhuria
Oktoberfest. Utamaduni wa sherehe hizo ni kuvaa kofia, kaptula na shati za
drafti pamoja na viatu aina ya buti, ambavyo vinakuwa na mwonekano kama askari
wa zamani.
Bayern ambayo inaongoza ligi ikiwa na
pointi moja mbele dhidi ya wapinzani wake wa jadi, Borussia Dortmund,
walionekana kuwa watulivu, huku kocha wao wakionekana kuwashangaza baada ya
kuzizoea sherehe hizo mahususi.
Si kucheza mpira pekee ambao
umewapatia ushindi katika mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Ulaya katika kundi D,
na ushindi wa kombe la Supercup dhidi ya Chelsea.
Bayern Munich wanaonekana kuzidi
kukonga nyoyo za mashibaki kuanzia uwanjani mpaka kwenye sherehe zao za
Oktoberfest.
Kwenye sherehe hizo kunakuwa na wake
zao, wapenzi wao, watoto, viongozi wa timu, wageni maalumu na waalikwa
mbalimbali ambao hujumuika na wachezaji wa Bayern Munich.
Sherehe za mwaka huu zimetimiza
miaka 180 tangu zilipoanza karne moja iliyopita.
OKTOBERFEST 16, WATU MILIONI 6
Utaona wake zao wamependeza, kocha
wao anafurahia, watoto wanafurahia, kumbe sherehe hizo zilianza miaka 180
iliyopita.
Kwa mara ya kwanza sherehe za
Oktoberfest zilianzia Kaefers Wiesenschaenke. Ni sherehe ya siku 16 ambazo watu
wanakula bata ndani ya Jiji la Munich, inaanza wiki ya mwisho ya mwezi wa tisa
kila mwaka hadi wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba.
Watu milioni 6 husherehekea kila
mwaka Oktoberfest, ambapo wenyewe huliita tamasha la ‘full bata” au “die
Wies'n” (Theresienwiese). Oktoberfest ilianza mwaka 1810, ni sherehe za
utamaduni kama ilivyo Samba Brazil.
Na mara nyingi zinafanyika wakati wa
mapumziko ya soka, ambapo timu za taifa zinacheza mechi mbalimbali.
Bayern Munich itacheza mechi ya Ligi
Kuu Oktoba 19, ambapo wataikaribisha Mainz kwenye uwanja wa Allianz Arena.
BATA NA KAZI
Wakati Guardiola akiwaongoza
wachezaji wake kula bata kwenye sherehe za Oktoberfest, baadhi yao 15
watalazimika kurejea katika timu za taifa.
Kati yao wachezaji 7 wa Bayern
Munich wameitwa katika timu ya taifa ya Ujerumani, ambapo wataichezea baada ya
kula bata kwenye Oktoberfest.
Winga Arjen Robben, anaamini kikosi
chao kina kiwango bora, na mapumziko yamewapa hamasa zaidi.
“Nina hakika wachezaji wa Bayern
tutafanya mambo mazuri na dunia nzima itafahamu zaidi. Baada ya sherehe hizi,
tutaingia uwanjani tukiwa na ari zaidi huku mashabiki wetu wakitupa hamasa, na
tutawafurahisha,” alisema Robben.
Hii si mara ya kwanza kwa Guardiola
kushiriki sherehe kubwa kama hii, lakini kocha huyo anaonekana kukubalika zaidi
kuanzia wachezaji, viongozi na mashabiki wa timu hiyo.
Wageni walioalikwa walijawa na hamu
ya kukumbatiana na Guardiola wakidai amewapa furaha tangu kuanza msimu huu.
BIA NA UBINGWA WA 23
Wachezaji wa Bayern Munich walikuwa
wakinywa bia ambazo zimesajiliwa kwa jina la Oktoberfest. Wote waliunganisha na
kusherehekea ubingwa wao wa 23, ambao waliutwaa msimu uliopita ndani ya uwanja
wa Allianz Arena.
Raha wanayopta Bayern Munich ni ya
kipekee, kwani wanasherehekea wakiwa wametulia kwa kila upande.
Ligi ya mabingwa wanaongoza kundi
lao. Ligi kuu Bundesliga wanaongoza na zaidi Oktoberfest ni kula bata la nguvu
kwa kwenda mbele.
No comments:
Post a Comment