BARCELONA,
Hispania
KLABU ya Barcelona imemtega kinda wa Manchester United, Adnan
Januzaj, baada ya kutangaza kuwa ipo tayari kumchukua iwapo atakataa ofa ya
kuongeza mkataba.
Kinda huyo mwenye umri wa miaka 18, amejipatia umaarufu
mkubwa, baada ya kufunga mabao mawili katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi
ya Sunderland Jumamosi.
Hata hivyo, Barca imekuwa ikifuatilia kipaji cha mwanasoka
huyo tangu hajajiunga na United kutoka Anderlecht mwaka 2011 na kwa sasa wanaamini
sana kwamba, Januzaj atahamia tu Nou Camp wakati atakapomalizia miezi minane
iliyobaki katika mkataba wake.
Katika hatua nyingine, Januzaj amefunguka
akisema kuwa itamchukua muda kabla ya kuamua
ni taifa gani achezee.
Kinda
huyo mwenye umri wa miaka 18, alisema jana kuwa kwa sasa anataka kuangalia
kibarua chake kabla ya kuamua kuichezea timu ya Taifa ya England.
Januzaj,
18 amekuwa gumzo tangu Jumamosi alipoiwezesha Man Utd kuibuka na ushindi dhidi
ya timu ya Sunderland.
Katika
mchezo huo, kiungo huyo ndiye aliyefunga mabao mawili yaliyoifanya timu hiyo
kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kumfanya kinda huyo aonekane kuwa mmoja wa wachezaji
chipukizi wenye kipaji cha hali ya juu barani Ulaya.
Januzaj
alizaliwa mjini Brussels na ana kila kigezo cha kuwa raia wa nchi hiyo, lakini
inaelezwa kuwa anaweza kuchukua uraia wa Albania kwa sababu baba yake alizaliwa
nchini humo.
Mbali
na nchi hizo, pia nyota huyo mwaka 2017 anaweza kupewa uraia wa England kama
atapewa kibali cha ukazi wa nchi hiyo na kocha wa Simba hao watatu anasema kuwa
anahitaji kupata msaada wa nyota huyo.
Januzaj
alishakataa wazi kuichezea timu ya Taifa ya vijana ya Ubelgiji na anasisitiza
kuwa chaguo lake ni kuichezea timu ya Taifa ya Albania.
Shirikisho
la Soka England, FA na kocha Hodgson wanahaha kwa sasa ili kuona kama kutakuwa
na uwezekano wa kumchukua kinda huyo, lakini yeye anasema kuwa anajisikia
mwenye furaha wakati akivuta muda.
“Kwanza nataka kuelekeza jitihada zangu kwenye
kile ambacho nakifanya Manchester United, kwa sababu kwa sasa hili ndilo jambo
la muhimu sana katika sehemu ya kazi yangu,” alisema kinda huyo.
Januzaj
alikiri akisema kuwa kwa sasa anachokitaka ni kufanya vizuri kwenye kikosi cha
Manchester United na alisema kuwa:
"Kwa sasa kuhusu soka la timu ya taifa siyo kitu ambacho nakiwazia sana.
"Nafahamu
kwanza napaswa kuelekeza jitihada zangu katika kile ninachokifanya Manchester
United kwa sababu kuanzia sasa ndicho
kitu muhimu katika kazi yangu,” alisema kinda huyo kabla ya kuongeza kuwa
anataka kuhakikisha anacheza vizuri na
kuifanyia kila kitu klabu hiyo.
Mbali na kauli za kinda huyo, pia wakala wake, Dirk De
Vriese ameshawaambia viongozi wa timu ya Taifa ya England kwamba wanapaswa
kusubiri.
No comments:
Post a Comment