Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, October 2, 2013

DROGBA: SIJAISHA NADHIHIRISHA HILO KWENYE MICHUANO YA VILABU ULAYA. NA WILFRED ZAHA KUELEKEA NEWCASTLE UNITED BAADA YA KUWEKWA KANDO KIKOSI CHA KWANZA UNITED.



 Didier Dragba amesema kuwa uhamisho wake wa mwezi Januari wa kujiunga na Galatasaray ulichagizwa na hamu yake ya kutaka kucheza tena Champions League barani Ulaya.

Mkongwe wa kimataifa wa Ivory Coast aliihama Chelsea na kuelekea Uchina wakati wa kiangazi mwaka jana 2012 baada ya kuisaidia Chelsea kutwaa taji kubwa la vilabu Ulaya mwezi Januari.

Galatasaray ilifika katika hatua ya robo fainali msimu uliopita na Drogba anataka kuonyesha kuwa bado yumo katika kiwango cha juu cha kucheza michuano hiyo.

"Nilipokuwa China nilikuwa ni waza kuwa bado nilikuwa na kitu cha kusema kuhusu soka la Ulaya" Amenukuliwa Drogba mwenye umri wa miaka 35 alipokuwa akiongea na Tuttosport.

"Sikuwa nimekwisha, nilikuwa na nguvu zote na nilitaka kutetea taji nililoshinda nikiwa na Chelsea. Nilidhani kuthibitisha ndani ya Champions League.

"Umri si tatizo bali ni namba. Kila kitu kinategemea ubora wako, uzoefu na afya.

Galatasaray inakibarua pevu dhidi ya Juventus usiku huu.

@@@@@@@@@@@@
WILFRED ZAHA KUELEKEA NEWCASTLE UNITED BAADA YA KUWEKWA KANDO KIKOSI CHA KWANZA UNITED.
Winga wa Manchester United Wilfried Zaha ameweka wazi kuwa klabu ya Newcastle ndio klabu ambayo anaweza kujiunga nayo endapo hatasalia katika klabu ya Manchester United.

Zaha hajacheza hata dakika moja katika kikosi cha kwanza cha United tangu mchezo wa ngao ya jamii pale United ilipoishinda Wigan Athletic katikati ya mwezi Agosti.

Newcastle, Swansea City, West Brom, Stoke City na klabu yake ya zamani ya Crystal Palace wote wameoinyesha kumuhitaji kwa mkopo katika nusu ya pili ya msimu.

Inaaminika kuwa Zaha na wawakilishi wake wanaitazama Newcastle kutoka sehemu za kaskazini/mashariki kuwa na nafasi wakati ambapo meneja wa United David Moyes akimuonyeshea taa ya kijani ya kuondoka kwa mkopo mchezaji huyo wakati wa uhamisho wa mwezi Januari.

Winga huyo alijiunga na United akitokea Palace mwezi januari kwa uhamisho wa pauni milioni £17 kabla ya kupelekwa kwa mkopo Selhurst Park katika kumalizia msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment