Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, October 28, 2013

AZAM YAISHUSHA SIMBA KILELENI BAADA YA KUIFUNGA 2-1 KWENYE MCHEZO WA LIGI KUU TANZANIA BARA ULIOCHEZWA UWANJA WA TAIFA


Beki wa Azam FC, David Mwantika (kulia), akichuana na mshambuliaji wa Simba, Ramadhani Singano katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Azam imeshinda 2-1.

Mshambuliaji wa Simba, Betram Mwombeki akiwatoka mabeki wa Azam FC.

Ramadhani Singano (kushoto), akimtoka David Mwantika. (Picha na Francis Dande)

Wachezaji wa timu ya Azam wakishangilia bao la pili la timu yao baada ya kuifunga Simba 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyikakwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Azam imeshinda 2-1.
Mashabiki wa Simba wakiwa wameduwaa huku wakifuatilia mchezo kati ya Simba na Azam FC.

Kipa wa Azam FC, Mwadin Ali akidaka mpira mbele ya mshambuliaji wa Simba, Sino Augustino.

Mshambuliaji wa Simba, Edward Christopher (kulia), akiwania mpira na wachezaji wa Azam FC, Kipre Tchetche na David Mwantika.
KIKOSI cha Simba leo imeonja uchungu wa kufungwa baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Azam FC mchezo uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba ambayo huu ndiyo mchezo wao wa kwanza kupoteza tangu kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara, bado ipo katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 20.

Simba ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa kiungo wake mshambuliaji, Ramadhani Singano ‘Messi’ dakika ya 13 akimalizia kazi safi ya Zahor Pazi aliyeitoka ngome ya Azam na kupiga krosi fupi iliyomkuta mfungaji.


Azam waliendelea kulisakama lango la Simba na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Kipre Tchetche dakika ya 45 akimalizia krosi safi ya Erasto Nyoni na kufanya timu zote kwenye mapumziko zikiwa zimetoshana nguvu kwa bao 1-1.

Kipindi cha pili mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa lakini Kipre aliizamisha jahazi la Simba baada ya kufunga bao la pili dakika ya 73 baada ya kufanya kazi kubwa ya kupangua ngome ya Simba na kumhadaa kipa, Abel Dhaira na mpira kujaa wavuni.

Kocha Mkuu wa Simba, Abdallah Kibadeni mara baada ya mchezo huo alisema amekubali matokeo hayo na kilisababisha ni kutokuwa na wachezaji wake nyota lakini makosa yaliyofanywa na wachezaji wake ndiyo yaliyosbabisha kupoteza mchezo huo.



VIKOSI:
Simba: Abel Dhaira, William Lucian, Issa Rashid, Hassan Khatib, Joseph Owino, Jonas Mkude, Ramadhani Singano, Said Ndemla, Betrum Mombeki, Zahor Pazi/ Sino Augustino na Amri Kiemba/ Edward Christopha.

Azam FC: Mwadini Ali, Erasto Nyoni, Wazir Salum, Aggrey Morris. Said Morad/ David Mwantika, Boluo Kipre, Salum Aboubakary, Humphrey Mieno/ Khamis Mcha, John Bocco, Kipre Tchetche na Joseph Kimwaga.

No comments:

Post a Comment