Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, September 12, 2013

UWANJA WA LAKE TANGANYIKA KIGOMA WAFUNGIWA SASA JKT KANEMBWA KUTUMIA UWANJA WA KAWAWA LIGI DARAJA LA KWANZA

Mechi za nyumbani za timu ya Kanembwa JKT ya Kigoma iliyoko Ligi Daraja la Kwanza (FDL) sasa zitachezwa katika Uwanja wa Kawawa badala ya ule wa Lake Tanganyika.

Uamuzi wa kuhamishia mechi hizo Uwanja wa Kawawa ulioko Ujiji umetokana na Uwanja wa Lake Tanganyika kutumiwa na Serikali katika Operesheni Ondoa Wahamiaji Haramu inayoendelea nchini kwa sasa. Uwanja huo hivi sasa unatumika kuhifadhi wahamiaji hao.

Kanembwa JKT inaanzia nyumbani kwa kuikaribisha Polisi Tabora. Mechi hiyo itachezwa Jumamosi (Septemba 14 mwaka huu).

No comments:

Post a Comment