Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, September 12, 2013

TEMEKE, MJINI MAGHARIBI KUCHEZA NUSU FAINALI COPA

Mshambuliaji wa Temeke, Hamis Msofe (kushoto) akijaribu kumtoka beki wa Iringa, Bashiru Yahaya (kulia) wakati wa mchezo wa robo fainali ya mashindano ya Copa cocacola iliyocheza jana kwenye Uwanja wa Karume, Ilala Dar es Salaam

Mshambuliaji wa Temeke, Saleh Omary, (kushoto) akijaribu kumtoka beki wa Iringa, Bashiru Yahaya (katikati) wakati wa mchezo wa robo fainali ya mashindano ya Copa cocacola iliyocheza jana kwenye Uwanja wa Karume, Ilala Dar es Salaam

Temeke na Mjini Magharibi zinapambana kesho (Septemba 13 mwaka huu) katika mechi ya nusu fainali ya michuano ya Copa Coca-Cola kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15 itakayofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, jijini Dar es Salaam.

Timu hizo zimetinga hatua hiyo baada ya kushinda mechi zao za robo fainali ya michuano hiyo zilizochezwa leo (Septemba 12 mwaka huu) asubuhi kwenye uwanja huo huo.

Wakati Temeke imetinga hatua hiyo baada ya kuilaza bao 1-0 Iringa lililofungwa dakika ya 18 na Ramadhan Mohamed, Mjini Magharibi imeing’oa Mtwara kwa ushindi wa bao 1-0.

Robo fainali nyingine zinachezwa leo (Septemba 12 mwaka huu) jioni kwa Kilimanjaro kuvaana na mabingwa watetezi Morogoro huku Arusha ikioneshana kazi na Ilala.

No comments:

Post a Comment