Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, August 11, 2013

YANGA MFENESINI KIBURUGWA WAFUNGUA TAWI LA YANGA

Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa klabu ya Yanga, Denis Oundo akifungua tawi la Yanga, la Mfenesini lililopo Mbagala Kiburugwa, jijini Dar es Salaam jana. Aliyepiga makofi ni katibu wa tawi hilo, Hafidh Limbanga.





MKURUGENZI wa Fedha na Utawala wa klabu ya Yanga, Denis Oundo jana alizindua tawi la Yanga, la Mfenesini lililopo Mbagala, jijini Dar es Salaam.

Denis Oundo ambaye alikuwa amefuatana na Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kiziguto na meneja wa timu ya Yanga, Hafidh Salehe walipokelewa kwa maandamano toka Mbagala hadi Kiburugwa huku wakiwa wamebeba kombe ambalo la Ubingwa la Yanga la 2012/13.

Akizungumza wakati akizindua tawi hilo, Oundo alisema anawapongeza wanachama hao kwa kuweza kuwa na wazo la kuwa na tawi kwani litakuwa kiungo kati ya wanachama na Makao makuu.
“Nawapongeza kwa kuanzisha tawi kwani itawasaidia ninyi kupata taarifa mbalimbali kupitia uongozi wenu hivyo wengine waige mfano wenu”, alisema Oundo.

Naye Makamu Mwenyekiti wa tawi hilo, Alphonce Rwena alisema wao wameanzisha tawi hilo ili lisaidie kuinua maendeleo ya klabu yao na kujenga umoja kwa wanachama.

“Sisi lengo letu kuanzisha tawi hili ni kujenga ushirikiano kati ya wanachama wa Yanga waliopo Kiburugwa na wanachama wengine na lengo lingine ni kuanzisha academi ambayo itakuwa inatoa wachezaji ambao wanaweza kusaidia Yanga”, alisema Rwena.

No comments:

Post a Comment