MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa
Ivory Coast, Gervinho amekamilisha rasmi usajili wake kutoka klabu ya Arsenal
kwenda AS Roma ya Italia kwa ada ambayo haikuwekwa wazi.
Gervinho mwenye umri
wa miaka 26 amefunga mabao 11 pekee katika miaka miwili ambayoamekuwepo Arsenal
na kushindwa kumshawishi kocha Arsene Wenger kumpatia namba ya kudumu katika
kikosi cha kwanza cha Gunners. Wakati Roma walipotangaza ofa yao ambayo
inakadiriwa kufikia kiasi cha euro milioni nane, Wenger alikubali haraka na
Gervinho kusafiri kwenda Italia mwishoni mwa wiki iliyopita kwa ajili ya
kufanyiwa vipimo vya afya na makubaliano binafsi. Akiwa Roma, Gervinho ataungana
na kocha Rudi Garcia ambaye alimfundisha wakati akiwa kinda katika klabu ya
Lille. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wake, Arsenal ilithibitisha
kumuuza mchezaji huyo Roma na kumshukuru kwa mchango wake katika kipindi chote
walichokuwa naye hapo.
Africa, Redefined: Mobila Safaris at Indaba 2026
-
The wait is over. Africa’s most iconic landscapes are calling, and we’re
here to hand you the keys.
*Mobila Safaris is officially live at Stand DEC...
KUMBUKIZI YA DARAJA LA NYERERE 2016-2026
-
Daraja la Nyerere lililozinduliwa na aliye kuwa Rais wa Tanzania John
Pombe Magufuli Aprili 19, 2016. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Picha za Viongozi mba...
WASIRA AWATOLEA UVIVU WALIOANZA MBIO ZA URAIS
-
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Stephen
Wasira, Leo Machi 27, 2026, Mjini Bunda Mkoa wa Mara alipokuwa akiweka
jiwe la ms...
Post a Comment