Kwa mara ya pili na kwa mwaka wa pili mahasimu wa soka la Misri Zamalek na Mabingwa watetezi Al Ahly wamewekwa tena katika kundi moja katika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani afrika maarufu kama Orange CAF Champions League katika ratiba iliyopangwa leo katika makao makuu yaCAF huko Cairo. Mafahali hao wawili wa Misri wapo kundi A na watakutana katika mechi ya ufunguzi wa makundi hayo ambayo ndiyo itakayo kuwa mechi ya kwanza 19-21st Julai huku Zamalek wakiwa wenyeji wa mchezo huo.
Mabingwa wa mwaka 1995 Orlando Pirates wataialika AC Leopards ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Congo katika mchezo wa kundi A .
Kocha msaidizi wa Zamalek, Ossama Nabuih amesema kuwa sio jambo la kushangaza kuwa kundi moja na mahasimu wao wakubwa Al Ahly kwa mara ya pili . “ tuliitarajia ratiba hii . hakuna kusema kuwa kundi hili ni rahisi au ngumu . Kwa hatua hii kila kundi ni gumu tuna kwenda kucheza kwa kujiamini na tutafuzu katika kundi hili ” . kundi letu ni gumu kuliko jingine . Tutakutana na timu ngumu kutoka katika mataifa tofauti .anamaliza Nabuih
Group A
Al Ahly (Egypt)
AC Leopards (Congo)
Orlando Pirates (South Africa)
Zamalek (Egypt)
Group B
Esperance (Tunisia)
Coton Sport (Cameroon)
Recreativo de Libolo (Angola)
Sewe Sport (Ivory Coast)
No comments:
Post a Comment