Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, May 17, 2013

SIR ALEX FERGUSON KUMALIZA MECHI YA 1500 KESHO AKIWA UGENINI WAKATI UNITED WAKICHEZA NA WEST BROM


JUMAPILI, MEI 19, ni Siku ya Mwisho ya Msimu wa BPL, Barclays Premier League, wa 2012/13 na Siku hiyo ndiyo Mechi ya 1500 kwa Sir Alex Ferguson akiwa Meneja wa Manchester United na ndio mwisho wa enzi yake kwa vile anastaafu.

Akiwa ametwaa Makombe 38 ndani ya Miaka 26 aliyodumu Man United, Sir Alex Ferguson, Miaka 71, amenena: “Ni Mechi 1500…Gemu yangu ya mwisho… inashangaza! Nataka kushinda hii kupita ile ya Wiki iliyopita!”

Jumapili iliyopita Sir Alex Ferguson aliagwa kwa shangwe walipocheza Mechi na Swansea City Uwanjani Old Trafford, ikiwa ni Mechi yake ya mwisho Uwanjani hapo, na kushinda Bao 2-1 na Jumatatu Timu nzima ya Man United ilitembeza Kombe la Ubingwa wa BPL kwenye Mitaa ya Manchester na kusindikizwa na Maelfu ya Washabiki hadi katikati ya Jiji, eneo la Albert Square, walipopokewa na Maelfu ya Umati.
Mwenyewe Ferguson amekiri kuwa mapokezi ya Wiki iliyopita yalishinda yale ya Mwaka 1999 walipopita Mitaani baada ya kutwaa Trebo, yaani Ubingwa wa England, FA CUP na UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, na kuweka Historia ya kuwa Klabu ya kwanza na pekee Uingereza kufanya hilo. 

Leo, kwenye Mkutano na Wanahabari kwenye Kambi ya Mazoezi ya Man United huko Carrington ambao ni kawaida ya kila Ijumaa kabla Mechi za Wikiendi, Wanahabari walimpa Sir Alex Ferguson zawadi ya Keki yenye umbo la Mashine ya Kukaushia Nywele ukiwa ni mzaha kuhusu imani ya kwamba Meneja huyo huwapa kibano Wachezaji wake wasipofanya vizuri na kuwafanya wajisikie vichwa vyao moto mithili ya kupitishiwa Mashine hiyo ya Kukaushia Nywele.
Akijibu kwa mzaha, Ferguson alisema: “Inastahili! Kuna wakati sikukubaliana nanyi na kile kilichoandikwa na kuna wakati mliandika vitu vizuri tu na nilividharau. Lakini Siku zote sikuweka kinyongo wala kisasi. Hiyo si staili yangu!” 

Ferguson pia alithibitisha kuwa Kipa Anders Lindegaard atakaa Golini Mechi na WBA na Masentahafu watakuwa Jonny Evans na Phil Jones huku Nemanja Vidic na Rio Ferdinand wakiwa Benchi akisisitiza sasa ni zama za Vijana.

Presence: Ferguson still held the power in the press conference, but looked more relaxed than usualrelaxed
Presence: Ferguson still held the power in the press conference, but looked more relaxed than usualrelaxed
Presence: Ferguson still held the power in the press conference, but looked more relaxed than usualrelaxed
Ferguson ameonekana wa furaha sana leo kwenye mkutano huo, huku akionekana mwingi wa ujuzi na kutaka kuonesha soka la ukweli mwisho wa msimu.

RATIBA-MECHI ZA MWISHO MSIMU HUU
Jumapili 19 Mei 

[Saa 12 Jioni] 
Chelsea v Everton
Liverpool v QPR
Man City v Norwich
Newcastle v Arsenal
Southampton v Stoke
Swansea v Fulham
Tottenham v Sunderland
West Brom v Man United
West Ham v Reading
Wigan v Aston Villa 



SIR ALEX - MAKOMBE AKIWA MAN UNITED 
LIGI KUU: 1993, 1994, 1996, 1997, 1999, 2000, 2001, 2003, 2007, 2008, 2009, 2011, 2013
FA CUP: 1990, 1994, 1996, 1999, 2004
LEAGUE CUP: 1992, 2006, 2009, 2010
UEFA CHAMPIONZ LIGI: 1999, 2008
UEFA KOMBE LA WASHINDI: 1991
FIFA CLUB WORLD CUP: 2008
UEFA SUPER CUP: 1992
INTER-CONTINENTAL CUP: 1999
FA CHARITY/COMMUNITY SHIELD: 1990, 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007, 2008, 2010, 2011

No comments:

Post a Comment