Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, May 4, 2013

HII NI SABABU MOJA INAYOFANYA ARSENAL WACHEKELEE BAYERN KUINYUKA BARCA



LONDON, England
KUNA sababu moja tu, kati ya nyingi inayofanya Arsenal kufurahia ushindi wa Bayern Munich dhidi ya Barcelona kwenye mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Arsenal na dunia nzima walishuhudia Bayern ikiitia aibu Barca, moja ya timu inayoaminika kuwa bora duniani, baada ya kuwatupa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya katika hatua ya nusu fainali kwa jumla ya mabao 7-0.

Barca ilifungwa 4-0 katika nusu fainali ya kwanza pale Allianz Arena wiki iliyopita, kabla ya Jumatano ya wiki hii, kunyukwa 3-0 nyumbani Nou Camp, na kuwafanya kuaga michuano hiyo kwa aibu kubwa hasa kwa timu kama Barca.

Sababu inayoifanya Arsenal kufurahia ushindi huo wa Bayern si kwamba kwasababu kuwacheka nyota wao wa zamani, Cesc Fabregas na Alex Song kwamba wamekumbana na kipigo, la bali jambo hilo litawaweka salama.
Kumekuwa na stori nyingi zinazozungumzwa kwa sasa kuhusu kocha mpya anayetarajia kutua Bayern msimu ujao, Pep Guardiola, kwamba moja ya wachezaji wapya atakaowataka watue Allianz Arena ni beki wa kati wa Arsenal, Laurent Koscielny.

Lakini, baada ya kutazama kiwango cha mabingwa hao wa Bundesliga katika mechi zake mbili dhidi ya wababe hao wa La Liga, Barca kumeonyesha matumaini makubwa kwamba Arsenal wataponyeka kwenye sakata hilo la Koscielny.

Pep ameitazama Bayern katika mechi hizo mbili za nusu fainali dhidi ya klabu yake ya zamani, hakuwa na mapokeo mazuri huku timu ya kwao, lakini ni wazi alifurahishwa na nguvu na ushupavu wa safu ya ulinzi ya klabu yake mpya ya Bayern.

Mabeki hao waliweza kutawala walipocheza dhidi ya timu ambayo inaaminika kabisa kuwa na safu hatari zaidi ya ushambuliaji katika historia ya soka, jambo ambalo linaondoa uwezekano mkubwa wa miamba hiyo kuingia sokoni kwa ajili ya kumsajili Koscielny, kwasababu ni dhahiri kabisa watakuwa hawamhitaji.

Barca na fowadi yao kali, ilicheza kwa zaidi ya dakika 180, lakini walishindwa kupata hata bao moja tu na kwenye mechi yao ya Jumatano usiku, ambapo walinyukwa 3-0, Bayern ilicheza bila ya beki wake bora kabisa, Dante, ambaye ni mgonjwa.

Jambo hilo linawashusha pumzi Arsenal, kwasababu Koscielny ameonekana kuwa kwenye kiwango bora kabisa kwa sasa, ameonyesha ubora ambao unaifanya Arsenal kuwa bora pia, hivyo kitendo cha kutokuwa naye beki huyo kutaifanya Gunners kuwa dhaifu.

Safu ya ulinzi ya Bayern ilionyesha bayana kabisa kwamba, ina nguvu ya kutosha na haihitaji kuongezwa mtu mwingine kama Koscielny, usajili ambao kama utafanyika basi utakuwa wa fujo tu ya kuitibulia Arsenal au kutaka kumweka pabaya Koscielny.

Koscielny kwa upande wake mwenyewe, kwa kiwango chake anaweza kudanganyika akataka kumshawishi wakala wake amtafutie dili mpya katika klabu hiyo, jambo hilo anaweza kulifanya lakini si kwa kutaka kujiunga na Bayern, kwasababu patakuwa mahali pagumu kwake kupata nafasi.
Moja ya tatizo kubwa linalomkabili kocha Arsene Wenger kwa miaka ya hivi karibuni ni kwamba, amekuwa anashindwa kuwalinda na kuwabakiza wachezaji wake bora pindi wanapotaka kuondoka.

Lakini, kutokana na kesi ya Bayern kuwa na safu bora kabisa ya ulinzi, huku hiyo ndiyo ikiwa ni timu inayotaka saini yake, hapa Wenger anaweza kushinda vita hiyo ya kumbakiza Koscielny.
Bayern ni timu ya Ujerumani ambayo imeruhusu mabao 14 tu msimu wote huu katika ligi yake ya ndani na mabao matatu tu ugenini, kitu ambacho kinatoa takwimu bora kabisa kwa timu hiyo inasafu bora kabisa ya ulinzi.

Koscielny ni beki bora, lakini kama Bayern itafikiria kuingia sokoni mwishoni mwa msimu na kusaka mchezaji mpya wa kuimarisha safu yao ya ulinzi, wanaweza kwenda kutafuta mtu mwingine sahihi zaidi kwa ajili ya timu yao.

Kwenye hili, Arsenal ipo salama katika mchakato wa kumbakiza Koscielny kwenye timu yao, kwasababu hataweza kuhamia kwenye timu ambayo hataweza kupata namba na pili Guardiola ana beki bora kabisa kwenye timu yake hiyo mpya ya Bayern, hatahitaji mtu mwingine kuongezeka.
Huu ni msemo wa kizamani sana, lakini unakubalika mahali hapa; kama fimbo bado haijavunjika, usitafute utaiungaje.

No comments:

Post a Comment