Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, May 16, 2013

DIAMOND PLATINUM KUONYESHA MAKALI YA BONGO FLEVA WAKATI NEY WA MITEGO AKIDHIHIRISHA HIP HOP NDIO HABARI YA MJINI DAR LIVE JUMAMOSI


Photo

Photo
MWAMUZIKI wa bongo fleva,  Nasib Abdul 'Diamond Platinum' amejigamba kumfunika Ney wa Mitego kwenye mpambano wao utakaofanyika Dar Live Mei 18, mwaka huu.

Akizungumza na LENZI YA MICHEZO, Diamond amesema anataka kudhihirisha kuwa muziki wa bongo fleva ni zaidi kuliko hip hop kuliko watu wanavyodhani wao wanaimba mapenzi tu na kubana pua.

"Nawaomba wapenzi wangu wote waje kwa wingi ili waone kazi yangu kwani naamini nitafunika na watapata burudani ya uhakika", alisema Diamond.

Mpambano huo umeandaliwa na kampuni ya YUNEDA inayosimamiwa na Kahabi Ngwendesha ili kuwapa burudani wakazi wa Dar es Salaam na kusaidia kuinua kipato cha wasanii

"Mpambano unaitwa ni muziki gani kwa maana ni muziki gani wenye mashabiki kati ya bongo fleva na hip hop ndio maana tumeamua kuwaweka Diamond na Ney wa Mitego jukwaa moja", alisema Kahadi.

Pia amesema kwa vile siku hiyo ndio ligi kuu inamalizika, anawaomba mashabiki wafike Dar Live wakamalizie sherehe za ubingwa kwani kiingilio ni 10,000 tu na kutakuwepo wasanii wengine watakaosindikiza mpambano huo.

No comments:

Post a Comment