Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, April 13, 2013

YANGA YAIVUA RASMI SIMBA UBINGWA BAADA KUIFUNGA JKT OLJORO MABAO 3-0


Kikosi cha Yanga

Kikosi cha JKT Oljoro

Hamis Kiiza akipambana na beki wa JKT Oljoro 

Nadir Haroub akikimbia baada ya kufunga bao la kwanza huku wachezaji wenzake wakimkimbilia




Beki wa JKT Oljoro Shaibu Nayopa akiondosha mpira eneo la hatari 




 TIMU ya Yanga leo imejikita kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Barabaada ya kuifunga JKT Oljoro mabao 3-0 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga imetimiza pointi 52 baada ya kucheza mechi 22, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 46, ambayo keshoitakuwa na kibarua cha kujiuliza kwa Simba zile bao 3-0 kwenye raundi ya kwanza zilikuwa halali
Hamisi Kiiza alipokea pasi nzuri ya Niyonzima na kumpiga chenga chenga kipa wa JKT kabla ya kuusukuma mpira nyavuni na bao la tatu dakika ya 43.

Bao la kwanza lilitiwa kimiani na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kwa kichwa baada ya mpira wa kona aliyopiga Haruna Niyonzima na kuokolewa na nahodha wa JKT Oljoro Shaibu Nayopa na kutua kichwani mwa Nadir Haroub na kuuzamisha kirahisi wavuni.

Simon Msuva alifunga bao la pili kwa shuti la mbali nje ya eneo la penalty  alipokea pasi maridadi ya David Luhende mabeki wa JKT Oljoro dakika ya 16

Mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda Hamis Kiiza alifunga bao la tatu baada ya kuwatoka mabeki wa JKT Oljoro na kumalizia na kumpiga chenga kipa na kufunga bao dakika ya 43 pia mchezaji Juma Abdul aliumia na kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Shadrack Nsajigwa.

Kipindi cha pili, baada ya dakika mbili tu Oljoro ilipata pigo baada ya kipa wake Mussa Lucheke kuumia na kumpisha Shaibu Issi  na alipoingia kipa huyu  Yanga walikosa mabao mengi ya wazi kwenye mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Amon Paul toka Mara akisaidiwa na John Kanyenye wa Mbeya na Arnord Bugado wa Singida.

Kikosi cha Yanga ni; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, David Luhende, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva, Frank Domayo, Hamisi Kiiza, Didier Kavumbangu na Haruna Niyonzima.

JKT Oljoro; Mussa Lucheke, Yussuf  Machogoti, Majaliwa Sadik, Nurdin Mohamed, Shaibu Nayopa, Salim Mbonde, Karage Mgunda, Emmanuel Memba, Paul Nonga, Iddi Saleh na Hamisi Saleh.

Huko Mbeya Tanzania Prison yaifunga  JKT Ruvu mabao 2-0 kwenye mchezo wa ligi Kuu uliochezwa uwanja wa Sokoine.

Ushindi huu umechagizwa na mashabiki wa soka wa mkoa huo kuanza kuichangia timu hiyo ili isishuke daraja wakiongozwa na Naibu Waziri wa Elimu, Mh. Mwilugo

No comments:

Post a Comment