Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, April 16, 2013

WATU WAWILI WAFARIKI BAADA YA KUTOKEA MLIPUKO WAKATI WA MBIO ZA BOSTON MARATHON JANA.

Watu na wanariadha wakikimbia kutoka mahala inayosemekana mabomu mawili yalilipuka moja baada ya nyingine

Wafanyakazi wa huduma za afya wakiwasaidia watu kwenye eneo la kumalizika mbiyo za Marathon ya Boston 2013
A runner in a wheelchair is taken from a triage tent after explosions went off at the 117th Boston Marathon in Boston, Massachusetts 

Mwanariadha wa kike ambaye jina lake halikufahamika mara moja akiondoka kwenye eneo la mashindano baada ya kutokea mlipuko

Mwanamke akiikumbatiwa na mwanamume anaemtuliza baada ya milipuko miwili karibu na hema ya huduma za dharura, Boston, Massachusetts

Polisi analinda eneo ambalo kuna hema ya huduma za dharura karibu na eneo ambalo mabomu yaluilipuka huko Boston

Wafanyakazi wa afya wakimbeba mtu aliyejeruhiwa upande wa pili wa tepu ya kumaliza mbiyo za Boston kufuatia mlipuko wa bomu

Milipuko miwili ya mabomu iliyotokea karibu na mstari wa kumaliza mashindano ya mbio za Boston Marathon, nchini Marekani imewauwa watu wawili na zaidi ya 50 wengine walijeruhiwa Jumatatu.

Maafisa wa usalama walisema mlipuko wa tatu ulitokea kwenye maktaba ya John F.Kennedy iliopo katika mtaa mwingine wa Boston. Hakuna majeruhi yeyote aliyeripotiwa kutokana na mlipuko wa tatu na bado haijafahamika vyema kama mlipuko huo unahusiana na milipuko miwili iliyotokea awali kwenye mji huo.
 
Polisi wa Boston hawakusema kama milipuko ilikuwa sehemu ya shambulizi la ugaidi. Msemaji wa polisi alisema timu ya wataalamu wa kutegua mabomu walikuwa wakichunguza mifuko na vifurushi  vilivyoachwa kiholela kwenye tukio la milipuko ya awali lakini hakuna vifaa vingine vyovyote vinavyohusiana na milipuko vilivyopatikana.
 
Picha za televisheni zilionesha matukio ya kuogopesha, mtaa ulijaa  vifusi na damu, wafanyakazi wa huduma za dharura wakiwa wamebeba machela waliwasili mara moja kwenye mahala  uharibifu mkubwa ulipotokea.
 
Milipuko ilitokea mmoja baada ya mwingine ikipishana sekunde chache tu karibu na eneo la kumaliza mashindano ya mbio ambayo yaliwashirikisha wanamichezo wapatao 27,000. Mashindano yalisitishwa baada ya milipuko kutokea pamoja na usafiri wa njia ya metro katika eneo hilo.
 
Rais Barack Obama amelihutubia taifa na kutoa rambi rambi zake kwa waathiriwa akiahidi kwamba wahusika wa tukio hilo watapatikana, watafikishwa mbele ya sheria na watafahamu kwa nini wamefanya kitendo hicho kiovu.

Wakati huo huo polisi nchini Ungereza wanasema wanatathmini mipango ya usalama kwa ajili ya mbio za marathon zitakazofanyika Jumapili mjini London, baada ya milipuko ya mabomu kutokea huko Boston na kusababisha vifo vya watu wasiopungua wawili.

Waandaaji wa marathon mjini London wanasema wamewasiliana na polisi kuzungumzia mipango ya usalama mara tu waliposikia tukio la milipuko la Boston nchini Marekani.
 
Maelfu ya wanariadha wamepangiwa kushindana katika mbio za London Marathon, zitakazofanyika chini ya muda wa wiki moja.

No comments:

Post a Comment