Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, April 16, 2013

UJUMBE WA FIFA WAANZA KAZI JAPO WASHINDWA KUONANA NA WAZIRI FENELLA MUKANGARA


MKUU wa Kitengo cha Uanachama wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Primo Corvaro aliwasili jana nchini tayari kutatua mgogoro wa Uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuanzia leo.

Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura amesema kwamba Primo aliwasili pamoja na Mkuu wa Kanda hii, Ashford Mamelodi na tayari wameshaanza kazi iliyowaleta ila wameshindwa kuonana na Waziri wa Habari,Michezo,Vijana na Utamaduni, Dr. Fenella Mukangara kutokana na kuwa kwenye vikao vya bunge la Bajeti linaloendelea Dodoma

Pia Wambura amesema ratiba nyingine inabaki kama ilivyopangwa awali kwa siku tatu na  ujumbe huo umeanza kukutana na Sekretarieti pamoja na Rais wa TFF na jioni hii utakutana na wagombea uongozi walioathiriwa na uamuzi wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF ambao wakiomba FIFA iingilie mchakato huo.

Majina ya wagombea wakaokutana na ujumbe huo na ratiba ni kama unavyoonekana kwenye majedwali yaliyopo chini.



ORODHA YA WALIOATHIRIWA NA MAAMUZI YA KAMATI YA RUFAA


NA.
JINA
NAFASI ALIYOGOMBEA
UAMUZI WA KAMATI YA UCHAGUZI
UAMUZI WA KAMATI YA RUFAA ZA UCHAGUZI
OMBI LA SHAURI KUANGALIWA UPYA AU UAMUZI WA KUKATA RUFAA FIFA
1.
Ahmedi Yahaya
Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu
Aloipitishwa
Aliondolewa
Aliomba shauri lake liangaliwe upya
2.
Mbasha Matutu
Ujumbe wa Kamati ya Utendaji (Mikoa ya Shinyanga na Simiyu)
Aliondolewa
Aliondolewa
Aliomba shauri lake liangaliwe upya
3.
Farid Salim Mbaraka Nahdi
Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF (Morogoro na Pwani)
Aliondolewa
Aliondolewa
Aliomba shauri lake liangaliwe upya
4.
Eliud Peter Mvella
Ujumbe wa Kamati ya Utendaji (Iringa na Mbeya)
Aliondolewa
Aliondolewa
Aliomba shauri lake liangaliwe upya
5.
Jamal Emily Malinzi
Urais wa TFF
Alipitishwa
Aliondolewad
Aliomba shauri lake liangaliwe upya na alikata rufaa FIFA
6.
Michael Richard Wambura
Makamu wa Rais wa TFF
Aliondolewa
Aliondolewa
Alikata rufaa FIFA



 PROGRAMU YA UJUMBE WA FIFA NCHINI

PROGRAMU YA SIKU TATU (Tarehe 15 – 18 Aprili 2013)



Date / Time

Activity
15 Aprili 2013
Saa 12:30 – 03:00
Kuwasili kwa wajumbe wa FIFA
15 Aprili 2013
Saa 04:00 – saa 05:00 usiku
Kikao na Rais wa TFF pamoja na Sekretarieti
16 Aprili 2013
Saa 04:00 – 05:00 asubuhi
Kwenda ofisini kwa Waziri wa Michezo kwa ajili ya kumsalimu
16 Aprili 2013
Saa 05:30 – 06:30 asubuhi
Kukutana na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kupata taarifa ya uchaguzi
16 Aprili 2013
Saa 06:30 – 08:00 mchana
Chakula cha Mchana
16 Aprili 2013
Saa 08:00 – 12:00 jioni
Kukutana na wagombea walioondolewa
17Aprili 2013
Saa 03:00 – 05:00 asubuhi
Kukutana na Kamati ya Rufa za Uchaguzi ya TFF
17 Aprili 2013
Saa 05:30 – 06:30
Mchana
Kupewa taarifa zinazohusiana na mchakato wa uchaguzi, i.e., kesi zilizo mahakamani

17 Aprili 2013
Saa 08:00 – 10:00 jioni
Kukutana na watu wengine ambao FIFA wanaweza kuomba kukutana nao
17Aprili 2013
Saa 10:30 – 11:00 jioni
Mkutano na waandishi wa habari – kushukuru mamlaka na pande zilizohusika kwa ushirikiano
18 Aprili 2013
Saa 10:00 – 12:00 Alfajiri
Kuondoka hotelini kwa ajili ya safari





No comments:

Post a Comment