Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, April 13, 2013

ROBERTO MANCINI AMCHEFUA SIR ALEX FERGUSON AAMUA KUMPASHA


Nonsense: Ferguson says that Mancini is wrong with his claim that teams roll over for Manchester UnitedMENEJA wa klabu ya Manchester United amempasha meneja wa mahasimu wao Manchester City, Roberto Mancini aliyedai kuwa United wanashinda mechi zao kirahisi kwasababu ya uwoga wa timu wanazokutana nazo. Mancini alimkasirisha Ferguson kwa kudai kuwa sababu kubwa ya United kufanikiwa kuongoza kwa pengo la alama 12 kwenye msimamo wa Ligi wa Kuu nchini Uingereza ni kwamba timu wanazokutana nazo huwa zinawahofia na kuamini kuwa hawawezi kushinda. Lakini Ferguson ambaye timu yake inaweza kuongeza pengo la alama kufikia 15 kama wakifanikiwa kushinda mchezo dhidi ya Stoke City Jumapili, ameeleza kuwa mara nyingi timu yake imekuwa ikipambana baada ya kutangulia kufungwa na kuibuka washindi kwenye mechi nyingi msimu huu hivyo hiyo ni sababu tosha kwamba Mancini hayuko sahihi. Ferguson amesema kauli ya Mancini haina maana yoyote kwa ligi ya Uingereza kwa miaka mingi imekuwa ni ligi inayoheshimika labda anatafuta wa kumlaumu baada ya timu yake kushindwa kufanya vizuri.

ROBERTO MANCINI KWA SASA ANALILIA FA CUP, ILI MSIMU UWE NA MAFANIKIO! 
Meneja wa Man City, Roberto Mancini, anaamini kuwa ushindi kwenye FA CUP utafanya Msimu wa Mancheser City uwe mafanikio.
Jumapili, Man City wapo Wembley kucheza Nusu Fainali ya FA CUP na Chelsea na Mshindi atatinga Fainali kuivaa Wigan ambao wametangulia leo baada ya kuifunga Millwall bao 2-0

Ingawa Wiki iliyopita Man City waliifunga Man United Bao 2-1 kwenye BPL, Barclays Premier League, lakini bado wako Pointi 12 nyuma ya Man United na Mechi zimebaki 7 tu.
Alipouliza kama kutwaa FA CUP na kumaliza Ligi nafasi ya Pili kutamaanisha nini kwa Man City, Mancini alijibu: “Ni muhimu kushinda Vikombe. Jumapli itakuwa ngumu lakini ni Mechi muhimu.’
Ikiwa Man City watatwaa FA CUP hilo litakuwa Kombe la 3 kwa Mancini katika Misimu yake mitatu na Klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment