Mshambuliaji wa Boom Fc Janker Ally akipiga shuti kwenye mchezo wa ligi daraja la pili uliochezwa uwanjaw a Makurumla Kinondoni huku |
Beki Rashid Juma wa Red Coast (njano) akiwania mpira na Barnabas Kanji (red) kwenye mchezo wa ligi daraja la pili uliochezwa uwanja wa Makurumla jana. |
TIMU ya Abajalo jana iliifunga Friends Rangers bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi Daraja la Pili Mkoa wa
Dar es Salaam hatua ya sita bora kwenye uwanja wa Kinesi.
Mchezo huo ambao ulikuwa
na ushindani kutokana na timu zote kucheza soka la uhakika lakini mabeki wa
Friends Rangers waliruhusu bao la mapema lililofungwa na Waziri Omary katika
dakika ya 35, bao ambalo lilidumu hadi mchezo kumalizika.
Kwenye Uwanja wa
Makurumla, Boom FC ilitoka sare ya bao 1-1 na Read Coast mchezo ambao ulikuwa
wa kuvutia kutokna na timu zote kucheza soka la kushambuliana kwa zamu dakika
zote.
Red Coast ndio walioanza
kufunga bao kupitia kwa Idrisa Pandu dakika ya 28 na Boom FC wakasawazisha
kupitia kwa Janker Ally katika dakika ya 41.
Uwanja wa Airwing, Sharif
Stars iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Day Break, bao hilo lilifungwa na
Dovan Kanyinda katika dakika ya 89.
Red Coast inaongoza ligi
ikiwa na pointi 8 ikifuatiwa na Abajalo yenye pointi 7 na Sharif Stars ina pointi
6 ambapo kila timu imecheza michezo minne na ligi hiyo itafikia
tamati Aprili 27.
No comments:
Post a Comment