Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, April 13, 2013

OMMY G AACHIA "MOLA NISAMEHE" BAADA YA KUOKOKA

MSANII Omary Mubba aka Ommy G, ambaye yupo kitambo kwenye muziki wa Hiphop Tanzania ameamua kumrudia Mwenyezi Mungu 'MOLA' baada ya kimya kirefu bila kuachia wimbo wowote wa Hiphop.

Akiongea na Lenzi ya Michezo amesema kuwa  "unajua huu muziki tunaofanya kiukweli hauruhusiwi ila tunafanya tu kwa ajili ya fedha na vitu kama hivyo"

Amesema amefanya nyimbo ya Hiphop inayoitwa "Mola nisamehe" katika Studio za Emotion chini ya usimamizi wa Prodyuza Kisaka akimshirikisha 'Salu B' na muda wowote utasikika katika vituo vya redio.

Ommy G anasema ameamua kumwimbia Mungu ili kuwakumbusha kwamba Mwenyezi Mungu yupo pia anawakilisha jamii ambayo imemsahau Mungu na  muziki una kazi ya kuelimisha na kuburudisha ila sasa imezidi kwani kila msanii  akiimba anaimbia Pombe na wanawake.

Pia amesema nyimbo hizo zinachochea Ongezeko la maasi duniani, na kupotosha maadili ya ki-Afrika.

Ommy G alivuma nyimbo za 'Hiphop Mdundiko', "Wambele mbele" na "Mtoto wa nyumba ile" ambapo nyimbo moja kati ya hizo ilikuwa-Nominated ktk Tuzo za muziki Tanzania japo hakufanikiwa kushinda Tuzo hizo.

No comments:

Post a Comment