Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, April 25, 2013

NYOTA WANAONGOZA KWA KUOLEWA NA KUACHWA


 MAISHA ya u-super star yana mambo mengi, watu maarufu duniani wamekuwa wakikumbwa na mikasa mingi na zaidi mikasa ya kimahusiano imekuwa mingi kiasi cha kuwachafulia kwenye masuala ya kijamii.
Kwa wanawake wenye umaarufu mara nyingi wamekuwa hawadumu kwenye mahusiano, hata hapa nyumbani Tanzania mahusiano ya watu maarufu yamekuwa kama ya kiti cha basi au gazeti  la mapokezi ambalo mtu yeyote ana haki ya kusoma.
Leo tunaangalia wanawake maarufu ambao wanaongoza kwa kuolewa na kupigwa talaka mara kwa mara.
Kerry Katona

Kerry Katona
Jina hili sio geni kwa wapenzi wa muziki wa R&B/Soul, kwani aliwahi kutamba sana akiwa na kundi la muziki la Atomic Kitten.
Kerry, ambaye alishawahi kuwa mke wa mwanamuziki Bryan McFadden kutoka kundi la Westlife, kwa sasa ni miongoni mwa nyota ambao leo hii wanajumuishwa katika chama hiki cha mastaa waliozoea kuolewa na kuachika.
Baada ya kuachana na Bryan alijivunia kwa kupata ndoa nyingine kwa Cabbie Mark Croft, hakudumu sana, aliachana naye na kisha hivi karibuni kutangaza ndoa na mchezaji wa zamani wa mchezo wa Rugby, George Kay.
Angelina Jolie
Angelina Jolie
Ukimchunguza Angelina Jolie unaweza kusema labda hafai kuwa mwanachama wa chama hicho. Huyu ni miongoni mwa watakaopokea ahadi mpya na kufunga pingu za maisha hivi karibuni tu.
Nyota huyo wa filamu nchini Marekani, Hollywood amekwisha kumuahidi mpenzi wake wa muda mrefu, mcheza filamu Brad Pitt kuwa watafunga ndoa mapema baada ya sheria ya mashoga kuoana kuhalalishwa kwenye Jimbo la California, nchini Marekani.
Angie na Brad walianza mahusiano yao wakati wakiwa katika kipindi cha utayarishaji wa filamu ya Mr & Mrs Smith, mwaka 2005, lakini kumbukumbu zinaonyesha Angie aliwahi kuwa kwenye mahusiano na Jonny Lee Miller mwaka 1994 na baadaye kufunga ndoa mwaka 1996.
Ukitaka kujua mapenzi ya Angie ni sanaa, wakati alipoolewa alivaa fulana nyeupe iliyoandikwa jina Jonny kwa damu yake, ikiwa ni sehemu ya kiapo cha mahusiano yao, ingawa hakuona aibu kung’ang’ania kuachika 1999, kisha kuolewa na Jonny Lee Miller mwaka 2000.

Ulrika Jonsson
Masikini Ulrika ni aina ya mwanamke ambaye naye hajachoka kujaribu kuwa kwenye mahusiano na mwanaume sahihi, ingawa kwa bahati mbaya mapenzi yake huangukia kwa wanaume asioweza kudumu nao.
Mlimbwende huyo mwenye asili ya Sweden aliwahi kufunga pingu za maisha na John Turnbull mwaka 1990 na ndoa kudumu kwa miaka mitano tu, hivyo alifunga ndoa nyingine mwaka 2003 na mtangazaji kutoka kituo cha matangazo cha MTV, Lance Gerrard-Wright.
Pengine nyota huyo (45) mwenye jumla ya watoto wanne na kila mmojawapo akiwa na baba yake, ni mwepesi wa kusahau maumivu ya mapenzi, kwani aliachana na Wright na kujitosa kwa kocha wa zamani wa England, Sven-Goran Erikkson, ambaye ni mwenye sifa ya kutembea na vimwana mbalimbali duniani kwa mahusiano ya muda mfupi na tena pasipo kujali utofauti wa umri.
Pamela Anderson
Pamela Anderson
Ni ngumu kuitaja orodha ya wanachama wa chama hiki pasipo kumtaja Pam, mcheza filamu mashuhuri aliyewahi kufunga ndoa na mpiga ngoma wa bendi ya zamani ya “Motley Crue,” Tommy Lee, baada ya masaa 96 tu ya kujuana kwao.
Faida ya ndoa yao ni kujirekodi mkanda wa ngono, kuzaa watoto wawili kisha kumwagana mwaka 1998.
Mwaka 2006 alifunga ndoa ya pili na mwanamuziki Kid Rock, ndoa iliyofanyika kwenye boti juu ya bahari ya Pacific kwenye fukwe ya St Tropez.
Pengine hufahamu ndoa hiyo ilidumu kwa muda gani, yaani ilikuwa mwaka mmoja tu, kwani Septemba 2007 alitangaza kuwa yupo kwenye mahusiano na mtayarishaji wa filamu, Rick Salomon, ambaye baadaye mwaka huo huo mwezi Desemba waliachana na kila mtu kuchukua maamuzi yake mengine.

Kate Winslet
Mcheza filamu huyo aliyekulia huko Reading Uingerza naye amekwisha kuolewa mara tatu, kigezo kinachomfanya ajumuike kwenye klabu hii.
Mwanamume wake wa kwanza alikuwa muongozaji na mtayarishaji wa filamu, Jim Threapleton, ambaye walianza mahusiano wakati wakiwa katika maandalizi ya filamu ya Hideous Kinky, mwaka 1997.
Wawili hao walifunga ndoa mwaka 1998 na kupata mtoto mmoja, lakini kutokana na umaarufu kuwa kiu yake, Kate alimbwaga Jim na kudondokea kwenye mahusiano ya mtayarishaji maarufu, Sam Mendes ambaye alimtoa Uingereza na kwenda kuishi naye New York.
Walifunga pingu za maisha huko Anguilla katika visiwa vya Caribbean kipindi akiwa na ujauzito wa mtoto wake wa pili, Alfie. Mwaka juzi Kate alidai talaka kutoka kwa Sam na sasa yumo katika ndoa na Ned Rocknroll, ambapo inaelezwa kuwa ndoa yao ilifungwa kwa siri kubwa mwishoni mwa mwaka jana.
Patsy Kensit
Nadhani kama chama hiki kitahitaji bingwa wao, bila shaka mkanda wa taji hilo wangempatia Patsy, ambaye ameshakaa kwenye ndoa za wanaume wanne hadi sasa.
Pengine muziki ndio chakula chake cha mapenzi, kwani mwanandoa wake wa kwanza alikuwa muimbaji Dan Donovan, aliyefunga pingu naye mwaka 1988, kisha muimbaji Jim Kerry aliyekula naye kiapo mwaka 1992.
Lakini kati ya wote hao, tunaamini mwanaume wake bora ni Liam Gallagher, ambaye walidumu muda mrefu toka mwaka 1996 hadi mwaka 2007 walipokuja kufunga ndoa, na mahusiano yao yalikuja kuvunjika baada ya Liam kutangaza kuwa aliwahi kumsaliti Patsy kwa kulala na Lisa Moorish kwenye wiki ya kwanza baada ya kufunga ndoa yao, jambo lililopelekea Lisa kushika ujauzito wa mtoto wake, Molly.
Dj Jeremy Healy ndiye mume wake wa nne, walioana mwaka 2010, lakini mapenzi yao hayakudumu muda mrefu, kitendo kilichomfanya awe mwenye kuchoshwa na kutokuwa na maisha ya ndoa kabisa.
Katie Price

Katie Price
Ni ngumu kuwataja wanamitindo wenye mvuto wa kimahaba duniani bila kumtaja Katie Price, maarufu kwa jina la Jordan.
Jordan ni chizi wa mapenzi, alianza kujulikana zaidi baada ya kuwa kwenye mahusiano na mcheza mpira Dwight Yorke na baadaye muimbaji Gareth Gates, muda mfupi baadaye alianza kuonekana na muimbaji raia wa Australia, Peter Andre, ambaye walifunga ndoa mwaka 2005.
Walianza familia pamoja, huku Peter akibeba jukumu la kumlea mtoto wa Yorke, Harvey kabla hawajazaa pamoja watoto wawili, Tiaamii na Junior.
Baada ya ndoa yao kuvunjika mwaka 2009 kwa madai kuwa Jordan aliwahi kumsaliti Peter kwa kutembea na Leo Penna, alifunga ndoa nyingine na Alex Reid mwaka 2010, ambayo ilivunjika mwaka huo huo.
Milionea huyo baada ya kukaa kwenye mahusiano mapya na Kieran Hayler, ambaye ni mcheza shoo za uchi kwenye klabu ya usiku, hatimaye wamefunga ndoa na kuna habari zimezagaa mitandaoni kuwa ni mjamzito.

No comments:

Post a Comment