Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, April 9, 2013

MSHAMBULIAJI MTUKUTU MARIO BALOTELLI AFUNGIWA MECHI TATU


STRAIKA  wa AC MILAN, Mario Balotelli, amefungiwa jumla ya Mechi 3 baada ya kulimbikiza Kadi za Njano 5 na pia kuwakashifu Waamuzi wa Mechi dhidi ya Fiorentina iliyochezwa Jumapili iliyopita. 


Wakati tayari akisubiri kuanza kutumikia Kifungo cha Mechi moja kwa kulambwa Kadi ya Njano ya 5 tangu aanze kuichezea AC Milan Mwezi Januari, Balotelli ameongezewa Kifungo cha Mechi mbili zaidi kwa kuwatukana Waamuzi wa Mechi hiyo na Fiorentina ambayo ilimalizika kwa sare ya Bao 2-2.

Kifungo hiki kitamfanya azikose Mechi za Ligi za Serie A dhidi ya Napoli Wikiendi ijayo na zile na Juventus na Catania ambazo zitafuatia.
Wachezaji wa AC Milan wakipongezana kwenye mtanange ambao Mario aliwapachikia bao chini

Mbali ya Kifungo hiki toka Chama cha Soka, Balotelli pia ana adhabu toka Klabuni kwake kwa kufumwa akivuta Sigara chooni ndani ya Treni iliyokuwa ikiwapeleka kwenye Mechi huko Florence.
Kuhusu Kifungo cha Mechi 3, AC Milan imethibitisha itakata Rufaa kupinga adhabu hiyo.

AC Milan inakamata nafasi ya 3 kwenye Serie A wakiwa Pointi 4 nyuma ya Napoli ambao wako Pointi 9 nyuma ya Vinara Juventus.
Kwa Mwaka 2013, Balotelli amepachika Bao 10 katika Mechi 11 alizochezea AC Milan na Timu ya Taifa ya Italy. 

No comments:

Post a Comment