Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, April 9, 2013

KOCHA BOBBY WILLIAMSON KIBARUA CHAKE CHAOTA MAJANI UGANDA


KOCHA wa timu ya taifa ya Uganda, The Cranes  Bobby Williamson ametimuliwa kibarua cha kuinoa timu hiyo baada ya kuifundisha kwa miaka minne na miezi nane. Shirikisho la Soka la nchi hiyo-FUFA lilithibitisha kumtimua Bobby Williamson katika kikao cha dharura walichokutana ingawa hakuna sababu haswa zilizotajwa ambazo zimepelekea kumtupia virago kocha huyo. Wlliamson mwenyewe alipotafutwa kuthibitisha taarifa hizo kwa njia ya simu alikubali kuwa ni kweli ameshapata barua ya kusitisha mkataba lakini alikataa kuongelea undani suala hilo akidai bado ni mapema. Kuhusu nani atachukua nafasi ya kocha huyo ofisa habari wa FUFA, Rogers Mulindwa amewaambia waandishi wa habari kuwa suala hilo litatuliwa na kamati ya utendaji itakapokutana ingawa hakuweka wazi ni lini haswa kamati hiyo itakaa.
Uamuzi wa FUFA kumtimua kocha huyo umekuja kufuatia kipigo cha mabao 2-0 ambacho Uganda imekipata kutoka kwa Liberia, kipigo ambacho kimeiacha timu hiyo mkiani katika kundi J la kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 wakiwa wameambulia alama mbili katika mechi tatu walizocheza.
Mashabiki wa Uganda

No comments:

Post a Comment