Msemaji wa GFA amesema katika michezo ya mwishoni mwa wiki wachezaji wa Ghana wameng’ara katika ligi mbalimbali za Ulaya ambapo washambuliaji Fred Benson, Ernest Asante, Asamoah Gyan na Prince Tagoe wote walizifungia timu zao katika ligi zinazoshiriki.
Pamoja na washambuliaji hao kung’ara, lakini pia wachezaji wengine wameng’ara katika timu wanazochezea, ambapo nchini England, Jeffrey Schlupp aliwika katika mchezo baina ya timu yake ya Leicester City dhidi ya Crystal Palace, ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 2-2, wakati Albert Adomah naye alifanya vizuri wakati timu yake ya Bristol City ilipotoa sare tasa dhidi ya Hull City.
Huko Ufaransa Andre Ayew naye aling’ara sana katika mchezo ambao alicheza sambamba na mdogo wake, Jordan Ayew na kuiwezesha Marseille kuilaza Brest bao 1-0. Kutokana na mafanikio ya wachezaji hao wa Ghana, GFA imetoa pongezi kwa wachezaji wote wanaocheza soka la kulipwa ambao wamekuwa na mchango mkubwa kwa klabu zao, kwani mafanikio ya klabu zao yanasaidia pia kuitangaza Ghana katika medani ya soka la Kimataifa
No comments:
Post a Comment