Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, April 21, 2013

CHALINZE WAFURAHIA MCHEZO WA NGUMI

Bondia Amos Thomas  kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Edrew Joseph wakati wa mpambano wa kuamasisha mchezo wa masumbwi Chalinze Mkoa wa pwani  Juzi mchezo huo ulitoka droo 

Baazi ya mashabiki wakiwa na Diwani wao
Bondia Said Minyusi wa Chalinze kushoto akirusha konde ambalo alina madhala kwa Zumbe Kukwe wa Dar wakati wa mpambano wa kuamasisha masumbwi Chalinze mkoa wa Pwani juzi  Kukwe alishinda kwa TKO ya raundi ya kwanza
Baazi ya mashabiki waliojitokeza kuhamasisha mchezo wa masumbwi wakiangalia burudani hiyo
Mabondia walio itimisha mpambano huo wakati wa kuhamasisha masumbwi Chalinze
Diwani wa Kata ya Bwilingi Chalinze Ahmed Kalama Nassar akizungumza kabla ya mpambano wa mwisho kwa ajili ya kuhamasisha ngumi katika kata hiyo
Mwaite Juma wa Chalinze kushoto akimwangalia bondia Mussa Ali baada ya kupiga konde zito na kwenda chini


ZAIDI ya mashabiki 300 wamejitokeza kuangalia mpambano wa Masumbwi kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa ngumi Chalinze  Mkoa wa Pwani pamoja na vitongoji vyake mashindano hayo ya masumbwi yaliyoandaliwa maalumu kuhamasisha mchezo huo katika vitongoji maarufu.
Uliwakutanisha mabondia wa Dar es salaam na Chalinze na mabondia wanaotamba katika kitongoji hicho mpambano huo wa masumbwi ulioanza saa tatu ya usiku na kumalizika saa nne na nusu uliwakutanisha bondia Amos Thomas aliye toka sare na Andrew Joseph huku mpambano mwingine ukiwakutanisha Zumbe Kukwe wa Dar es salaam aliye mgalagaza bila huruma Said Minyusi wa Chalinze
Mpambano mwingine ni Alex Kado wa Chalinze alishindwa kuhimili mikiki mikiki ya Nassoro Khatibu na kupigwa kwa pointi
Pambano lililokuwa likisubiriwa na watu wengi zaidi ni mpambano uliowakutanisha Mwaite Juma wa Chalinze na Mussa Ali ambapo Mwaite aliweza kumsambaratisha Ali kwa TKO ya raundi ya kwanza na kupeleka shwangwe kwa wapenzi waliojitokeza katika mpambano huo
Baada ya kumalizika kwa mpambano huo Diwani wa Kata ya Bwilingi Chalinze Ahmed Kalama Nassar ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mpambano huo alisema yupo tayari kuwanunulia vifaa vya mchezo huo ili kuendeleza masumbwi katika kata hiyo
Ambapo ameahidi kuongeza ushirikiano wa wataalamu wa masumbwi kwa kushirikiana na viongozi ili Chalinze kiwe kitovu cha masumbwi nchini

No comments:

Post a Comment