Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, April 11, 2013

AZAM YAIWASHIA INDIKETA YANGA, SASA PENGO NI POINTI 3, JUMAPILI KUPAMBANA NA SIMBA



AZAM FC leo imejiongezea pointi tatu baada ya kushinda mabao 3-1 dhidi ya African Lyon kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.


Kwa matokeo hayo Azam FC imepunguza pengo la pointi sita ilizokuwa inazidiwa na vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC na  kubaki tatu huku jumapili ikishuka dimbani kucheza  na Simba.
Mabao ya Azam yamefungwa na Khamis Mcha dakika ya tisa na Kipre Tchetche dakika za 28 na 61, wakati la Lyon lilifungwa na Adam Kingwande dakika ya 36.

Kipigo hicho kinazidi kuiweka Lyon katika hatari ya kushuka daraja, ikiwa na pointi zake 19, baada ya kucheza mechi 23 huku wachezaji wake leo wakionekana na staili mpya za nywele.
Kikosi cha Azam kilikuwa; Aishi Manula, Himid Mao, Wazir Salum, Luckson Kakolaki, Joackins Atudo, Jabir Azizi, Kipre Tchetche, Abubakar Salum, Abdi Kassim, Ibrahim Mwaipopo na Khamisi Mcha.
                                                             
African Lyon; Noel Lucas, Ibrahim Isaac, Sunday Bakari, Yussuf Mlipili, Obinna Salamusasa, Juma Seif, Jackob Massawe, Mohamed Samatta, Adam Kingwande, Freddy Lewis na Ndela Kashakala


 Wachezaji wa Azam FC wakishangilia jushindi wa timu yao baada ya kuifunga African Lyon mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam.
Mashabiki wa Azam FC wakiishangilia timu baada ya kuifunga African Lyon mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment