Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, March 3, 2013

SIMBA YACHEZEA KICHAPO 4-0 KWA LIBOLO, JAMHURI YA PEMBA NDIO USISEME YALALA KWA 5-0 ILA AZAM LAMBALAMBA ZAO ZAZIDI KUWANOGEA WASUDAN WALAMBA 5-0


Azam ikipambana na Al Nasir wakati wa mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa



Wakililishi wa Tanzania , timu ya Jamhuri ya Pemba, imekuwa timu ya kwanza ya Tanzania kutolewa kwenye michuano ya Afrika, kwa kufungwa mabao 5-0 na Kedus Giorgis ya Ethiopia kwenye mchezo wa marudiano wa raundi ya kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika.

Matokeo hayo Jamhuri itakuwa imeaga kwa kufungwa mabao 8-0, baada ya mchezo wa kwanza kufungwa 3-0 katika Uwanja wa Gombani, Pemba.
Simba ambayo ni wawakilishi wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kukubali kufungwa mabao 4-0 na wenyeji Recreativo de Libolo mjini Calulo nchini Angola.

Simba imekubali kipigo hicho ikiwa na mlinda mlango wake Abel Dhaira mpaka mapumziko walishafungwa bao 1-0 na matatu yalifungwa kipindi cha pili. Kwa matokeo hayo Simba imeaga kwa kipigo cha mabao 5-0.

Wawakilishi wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho, Azam FC wao wanaendelea raundi ya pili baada ya kuifunga Al- Nasri ya Juba au unaweza kuita Sudan  Kusini mabao 5-0
Mabao mawili yamefungwa kipindi cha kwanza na matatu yamefungwa kipindi cha pili na Hamis Mcha mawili, John Bocco Adebayor mawili na Kipre Tchetche moja.

Kwa matokeo hayo Azam wanasonga mbele kwa jumla ya mabao 8-1, mabao 3-1 waliifunga kwenye mchezo wa nyumbani

No comments:

Post a Comment