Sunday, March 3, 2013
ABEL DHAIRA WA SIMBA LEO KUSIMAMA LANGONI DHIDI YA LIBOLO
"AMA KWELI MVUMILIVU HULA MBICHI"
HATIMAYE kipa Mganda, Abbel Dhaira Simba SC leo atakaa langoni katika mchezo wa marudiano wa Raundi ya Kwanza, Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji wa Recreativo de Libolo, utakaopigwa kwenye Uwanja wa Manispaa mjini Calulo, Angola.
Taarifa ambazo Lenzi ya michezo imezipata kupitia afisa habari wa Simba, Kwanza Lul Angola, zinasema kocha wa Simba, Mfaransa Patrick Liewig alisema beki wa kulia atakuwa Nassor Massoud ‘Chollo’, kushoto Amir Maftah, wakati katikati Komabil Keita na Shomary Kapombe.
Safu ya kiungo ni Amri Kiemba nyuma, Abdallah Seseme, kushoto na kulia Haroun Chanongo na Salim Kinje na mshambuliaji atasimama Felix Sunzu peke yake.
Mwinyi Kazimoto ambaye anasumbuliwa na maumivu ya jino anaanzia benchi, Juma Kaseja yuko fiti kabisa, lakini Liewig amempumzisha
Ikumbukwe, Simba iliyofungwa 1-0 katika mchezo wa kwanza mjini Dar es Salaam, inahitaji ushindi wa 2-0 ili kusonga mbele.
KIKOSI cha Simba leo Abbel Dhaira, Nassor Massoud ‘Chollo’, Amir Maftah, Komabil Keita, Shomary Kapombe, Amri Kiemba, Abdallah Seseme, Haroun Chanongo, Felix Sunzu na Salim Kinje.
BENCHI; Juma Kaseja, Juma Nyosso, Kiggi Makassy, Mwinyi Kazimoto, Mrisho Ngassa, Ramadhani Chombo ‘Redondo’ na Abdallah Juma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment