Rais Tenga akisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) |
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewasilisha rasmi maombi ya kuonana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara ili kuzungumzia uamuzi wake wa kutengua usajili wa Katiba ya 2012.
Maombi hayo yaliwasilishwa rasmi Wizarani Machi 4 mwaka huu ambapo TFF imependekeza kikao hicho kifanyike kesho au Machi 13 mwaka huu.
Kamati ya Utendaji ya TFF iliyokutana Machi 2 mwaka huu kujadili tamko ya Waziri kutengua matumizi ya Katiba ya 2012 ndiyo iliyopendekeza kikao hicho kwa lengo la kusikiliza upande wa TFF katika suala hilo.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment